Unknown Unknown Author
Title: RIWAYA: SITAISAHAU FACEBOOK SEHEMU YA KUMI NA SITA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
SITAISAHAU facebook MTUNZI: Emmy John Pearson. MAWASILIANO: 0654 960040 SEHEMU YA KUMI NA SITA Badala ya maumivu nikakumbana na yowe kubwa k...

clip_image003SITAISAHAU facebook
MTUNZI: Emmy John Pearson.
MAWASILIANO: 0654 960040
SEHEMU YA KUMI NA SITA
Badala ya maumivu nikakumbana na yowe kubwa kutoka kwa daktari. Nilipogeuka na mimi nikiwa na hofu nikamkuta amekaa chini. Mbali na mimi. Alikuwa ana hofu!! Jasho likimtoka.
“Daktari!!.” Nilimuita. Hakunijibu, alikuwa katika mshangao. Alikuwa akinitazama kwa wasiwasi.
Nilikuwa siijui tena thamani ya kuwa na mavazi na aibu ya kuwa uchi. Nilitapatapa hivyohivyo pale ndani. Daktari akiwa bado ananishangaa.
“Vaa nguo!” aliniamuru kwa sauti ya chinichini. Nikaziendea nguo zangu na kuzivaa.
Kisha nikamfuata hadi ofisini!
“Chukua pesa zako!!” alinikabidhi pesa zile. Nilisita kuzichukua akanisihi nizichukue. Nikatii!!
Nini kimetokea daktari? Nilimuuliza. Hakunijibu bali alisikitika.
Kisha akaanza kunielezea juu ya nini alichokiona. Ilikuwa ni alama ya maajabu katika mwili wangu sehemu za makalio. Mwili wangu ulikuwa umetoboka na matundu hayoyaliweza kuonyesha alama ya ‘666’.
Mungu wangu!! Nikashangaa, daktari yeye akawa ni wa kusikitika tu!
“Usipokuwa mkweli utakufa wewe na familia yako nzima kama wenzako.”
“Wenzangu? Wapi”
“Mnaomtumikia”
“Nani?” nilihoji kwa hofu.
“Mmiliki wa hiyo alama. Kwani siku wanakuwekea hawakukuambia.” Alinihoji kwa utulivu mkubwa.
Nikawa kama mwendawazimu na sikuwa na lolote ninalojua kuhusu hiyo alama katika makalio yangu.
“Daktari sijui lolote mbona.”
“Haya shauri zako, atakufa mama, baba, mdogo wako, dada, shangazi, mjomba, wifi, na marafiki ikibidi kisha watakumalizia wewe tena kwa uchungu mkubwa.” Daktari alinieleza haya kama simulizi ya kawaida huku akinitajia orodha ya watakaokufa. Kwa lugha nyepesi alikuwa kama babu anayemsimulia mjukuu simulizi ya kutisha. Nikatetemeka sana!! Vifo!!
“Sasa daktari jamani mimi ninakuficha nini. Mimi sijui kitu.” Nilishindwa kuendelea kuongea nikaanza kulia. Nililia sana maana nilikuwa nimekata tamaa. Mbaya zaidi nilikuwa nimepigwa chapa ya 666.
“Ndio maana nimejishangaa sana, iweje leo nikubali kuchukua rushwa, nikubali kutoa mimba msichana. Ama kweli kila mwenye alama hii hatakataliwa na dunia kwa lolote.” Daktari alinong’ona kama anasema mwenyewe vile. Nilisikia kila kitu.
Sasa nilikuwa nimechanganyikiwa!
“Nitakusaidia.” Alinyanyua uso daktari akanieleza huku akinitazama vyema usoni.
Nilifarijika sana kusikia maneno yale. Kisha akaendelea, “Lakini uwe mkweli kwa kila kitu. Ukijaribu tu kuficha lolote lile. Nasema ukijaribu kuficha lolote lile. Wewe, marafiki na ukoo wako wote utatokomea. Mimi nakueleza haya kama mzee wako, katika kipindi changu cha miaka ishirini ya udaktari nakutana na matukio mengi. Lakini hili ni la tatu katika maisha yangu. Wenzako wawili, mmoja miaka saba imepita na mwingine mwaka juzi, nilitaka kuwasaidia lakini wakaleta ujanja ujanja. Tuliwazika!! Aah!! Hatukuwazika insearch labda niseme tuliyafukia mabaki yao.” Alimaliza kunielezea kisha akashusha pumzi kali sana.
Macho yangu nilihisi kama yanajilazimisha kutazama mbele. Machozi yalikuwa yamezidi. Mapigo ya moyo yalikuwa juu, sasa nikaanza kuamini niliyokuwa nayatazama katika filamu za kinaijeria. Kumbe uchawi upo? Hakika uchawi upo!!
“Kesho njoo!!” alinipa ahadi hiyo.
“Kwa hiyo sitatokwa damu tena?” niliuliza swali la kijinga.
“Kwani mimi ndiye niliyekuwekea” Daktari naye akanipa jibu la kijinga kama nilivyotegemea.
“Usimwambie mtu yeyote kuhusu maongezi haya.” alinionya
Nikaaga! Kiguu na njia hadi nikaipata taksi.
Njia nzima nilikuwa nawaza na kuwazua. Zile ndoto zangu za kumjengea mama nyumba nzuri, wadogo zangu kusoma shule za kimataifa, mimi kuwa maarufu zaidi chuoni, ndoto za kwamba nataka kuwa mtakatifu! Zote zilikuwa zimekufa. Sasa nilikuwa nahangahika huku na huko huku nikisurubika na mateso ya nafsi.
Swali likajengeka katika kichwa changu. Dokta Davis linizuia nisimueleze mtu kuhusu mambo haya. Sasa daktari ananisihi nisifiche kitu. Hapa sasa nimuamini nani? Nilijiuliza.
“Kata kushoto!!” nilimuelekeza dereva.
Mawazo yangu yakawa yameishia hapo.
Maria aliniona kuanzia mbali. Akanikimbilia, akafika akanikumbatia.
“Da Bela jamani. Mbona mnyonge hivyo!.”
“Nimemkumbuka sana John.” Nilidanganya, huku siri kubwa nikiwa nayo mwenyewe.
Maria akaniongoza hadi ndani. Nikajibweteka kwenye sofa sebuleni. Maria akaniletea maji ya matunda niliyokuwa nayapenda, nikayagida kwa fujo kisha nikagundua kuwa nilikuwa na njaa. Chakula kilikuwa tayari!! Maria akanihudumia. Sasa niliweza kupumzika!! Sikutaka kwenda chumbani. Nililala sebuleni.
Kila baada ya masaa kadhaa nilikuwa naamka na kubadilisha pedi na nguo ya ndani kisha kuoga. Hali hii japo ilikuwa haijatimiza hata mwezi kwangu ilikuwa mateso makubwa. Sasa sikuweza kwenda kwa marafiki wala nisingeweza kwenda. Nilijihisi ninanuka, japo Maria hakuwa ameniambia hata siku moja lakini nilijijua mwenyewew kuwa sikuwa kawaida hata kidogo.
Siku hii ikamaliza bila tatizo!!
(MATESO YA 666)
Asubuhi ya siku iliyofuata niliwahi sana kuamka. Badala ya kumuomba Mungu anijalie uzima na aniepushe na matatizo haya mimi niliwekeza imani yangu yote iliyosalia kwa daktari yule ambaye hadi sasa sikuwa namfahamu jina lake.
Saa nne kamili asubuhi. Nilikuwa katika mlango wa kuingia ofisini kwake. Japo kulikuwa na watu kadhaa waliohitaji kuonana naye. Mimi nilipewa kipaumbele, nikawapita nikaingia ndani.
Ahaaa!! Binti! Vipi kwema? Alinichangamkia sana. Nikamjibu salamu yake. Nikakaa kitako kumsikiliza.
“Ngoja niwaondoe hawa watu hapo nje. Wewe nitakupigia simu uje mahali.” Alininong’oneza. Nikamuelewa nikampatia namba yangu ya simu kisha nikaaga.
****
Sikuchoka kusubiria. Japo alichukua muda sana. Baada ya masaa mawili na nusu. Aliniita odisini kwake. Nikaenda upesi nikamkuta akiwa pamoja na mwanaume ambaye laiti kama ningekutana naye wakati ule ambao nilikuwa na jeuri ya pesa sidhani kama alikuwa na hadhi ya kupokea salamu yangu. Nilimsalimia kwa kuwa tu alikuwa pamoja na daktari.
Nilipomsalimia badala ya kunijibu, akanikonyeza!! Nikataka kusonya nikasita.
Kwa ncha za macho yangu nikamtazama mwanaume huyu, kuanzia mavazi yalivyochoka, amechakaa nywele zake na hata ngozi ilikuwa imepauka. Nikaamini hata akili yake haiku sawa. Nilipokumbuka jambo hili la akili kutokuwa sawasawa nikaamini atakuwa ni mgonjwa wa akili. Na daktari huyu alikuwa katika kumpa tiba. Kimoyomoyo nikamsamehe kwa kosa la jinai alilofanya la kunikonyeza.
“Binti..kama nilivyokueleza jana!! Usisite kuusema ukweli wote. Ukificha haitakusaidia kitu zaidi ya kuuangamiza ukoo wako wote.” Alinieleza kwa utulivu. Yule tahira akacheka.
“Sawa daktari.” Nilimjibu. Tahira akacheka tena!! Akaanza kunikera.
“R.I.P mtu wako niliyekwambia ndio huyu.” Sasa daktari hakuwa akizungumza na mimi, bali alikuwa akisemezana na yule tahira. Nikashtushwa na hali ile, ina maana ananikabidhi mimi kwa yule chizi au alikuwa anamtania. Niliomba iwe hivyo lakini haikuwa. Alimaanisha.
Sasa tahira akanivagaa akanishika mikono. Nikajitoa mikononi mwake akacheka!!
“Nenda naye ofisini kwake huyo akakupe maelekezo. Anaitwa R.I.P”
“Na yeye anaitwa nani.” Yule mtu niliyedhani ni tahira sasa aliuliza.
“Jitambulishe binti.” Tahira alinieleza huku akinishika makalio. Kidogo nimtukane. Nikasita baada ya kuona daktari hakushtushwa na jambo hilo.
Nitafanya nini sasa!! Nikaanza kufuata uelekeo alionipeleka. Mara kwa mara alikuwa anacheka. Tulipishana na watu wengi lakini hakuna aliyemshangaa. Huyu sio tahira!! Nililazimika kuamini
Mlango ukafunguliwa nikaingia ndani!! Ofisi yake ilikuwa na hewa nzito sana ya madawa lakini yeye aliifurahia.
Karibu ukae…aaah!! Usikae kwanza hebu njoo huku.” Akanivuta kwa nguvu, nikamfuata. Akafungua kabati moja kwa fujo sana.
Mungu wangu!! Maiti!! Nikaruka pembeni kwa uoga huku nikitaka kukimbia, akacheka!!
“Binti hawa nao walikuwa wajinga wajinga tazama….njoo..njoo” akaniita huku akitabasamu. Nikasogea.
Akavuta kabati jingine likafunguka.
Maiti ya mwanamke. Akamgeuza. Alikuwa na alama ya 666 katika makalio yake. Maiti huyu nilikiri kuwa kabla ya kuwa hivi alikuwa mrembo sana maana licha ya kuwa maiti tayari bado alikuwa anavutia kumtazama. Alikufa huku anatabasamu.
Sijui nini kilimuua maskini!!
Akanipeleka katika kabati jingine akavuta tena. Akatoka mtoto mdogo. Hana kichwa na yeye ana alama ya 666..R.I.P kazi yake ilikuwa kucheka tu kama tahira. Wakati mimi nilikuwa katika hofu kuu. Hofu ya kukutana na maiti.
Sasa nilikuwa nimechanganyikiwa. Maiti karibia tano zilikuwa pamoja nasi, waziwazi. Amani ikatoweka moyoni.
“Na wewe ukificha neno lolote tu!! Utakufa na vizazi vyote vitakavyofuata.” Aliongea bila kucheka sasa.
Nilikuwa natetemeka.
“Hata huyo uliyemkalia na yeye nadhani ni walewale..hebu funua.” Alinambia huku akikazia macho mahali nilipokuwa nimeketi.
“Wapi?” nilimuuliza, likiwa neno langu la kwanza hapo ndani.
Akanionyesha kwa kidole. Ni pale nilipokuwa nimekaa. Nikafunua nikiwa natetemeka.
“Mamaaa!!” nikapiga kelele. Kumbe nilikuwa nimekaa juu ya maiti. R.I.P akacheka sana huku akirukaruka!!
Zile dharau zangu zikawa zimeishia hapa!! Nikamuheshimu!!!
R.I.P hakujali kama nilikuwa nimeshtuka ama la! Aliendelea kuongeaongea huku akiwatukana matusi mazito ya nguoni wale maiti kama vile wanamsikia. Hakika alifanana na mtu aliyerukwa akili. Kuishi na maiti napo kazi sana huenda ndo maana amechanganyikiwa.
“Ulisema unaitwa nani vile.”
“Naitwa Isabela.”
“He!! Unaitwa Isabela, yupo mwenzako humu hebu njoo umuone.” Akanivuta kwa kutumia nguvu sana hadi mkono ukashtuka. Yeye hakujali hayo. Akanivuta vuta hadi tukafikia kabati jingine. Nikajiandaa kushuhudia maluweluwe mengine.
Vuu!! Akafungua!!
“Hili nalo lilikuwa linakula nini sijui likanenepa hivi. Majitu mengine mapumbavu sana ujue. Heri yako wewe haujanenepa sana. Yaani hili lilikuwa limeridhika kweli dah!!” Alizungumza peke yake. Kisha kama kawaida akaitukana ile maiti.
Akatumia mikono miwili akavuta. Likatoka bonge la mwanamke. R.I.P akaanza kucheka, kicheko kikubwa hadi akatoa machozi.
“Anaitwa Isabela huyu, mpumbavu sana huyu alienda kunenepeana huko. Amewasumbua sana siku ya kumleta humu ndani. Kuna vindugu vyake, vyembamba hivyo basi likawa linawaponyoka. Linaanguka puu!!”alisimulia huku anacheka. Mimi sikuwa namuelewa anachomaanisha.
Kisha tukarejea tena mahali tulipokuwa nikalazimika kukaa juu ya lile jokofu la kuhifadhia maiti. Ningefanya nini sasa!!
“Au nimlete Isabela mkae nae, Isabela bonge.” Aliniuliza. Mimi nikawa namshangaa. Yaani alikuwa kama mpumbavu fulani.
“Isabela….umewahi kufa wewe?” aliniuliza.
Swali gani sasa hili la kijinga!! Nikawaza.
“Bado”
“Mwenzako niliwahi kufa. Na wewe una hamu ya kufa.”
He!! Umewahi kufa….kivipi.”
“Kwani mtu akifa anakuwaje? We naye unataka kuwa lijinga kama Isabela bonge” aliniuliza, sikujibu. Akanitukania mama yangu!!!
R.I.P alikuwa wa aina yake!!
Akaendelea, “hebu tuachane na hayo..msichana mdogo kama wewe ukifa sio vizuri ujue. Yaani hadi dhambi!!”
“Kama ukiwa makini hautakufa. Tena wewe hautakufa, nitakusaidia usife sawa!!”
“Sawa!!” nilijibu kwa nidhamu kubwa.
“Njoo huku…”
Nikamfuata hadi mahali patulivu kabisa. Sasa hii ilikuwa ofisi kweli. R.I.P akanipokea. Akaniacha ofisini kwa muda, kisha akaingia tena baada ya dakika kadhaa.
Hakuwa yule tahira, hakuwa mchafumchafu kama nilivyokueleza mwanzoni. Huyu alikuwa na hadhi ya yule mvulana ninayemuhitaji. Alikuwa mtanashati.
Hakuwa akicheka hovyo! Alikuwa makini na mtaratibu.
Roho Iliyo Potea (R.I.P). Alianza kwa kujitambulisha jina lake halisi. Kisha akanipongeza sana kwa ujasiri wangu hadi kufika hapo.
Akajieleza kwa ufupi maisha yake ya utafutaji huku na kule hadi alipojikuta akitafuta kwa njia za mashetani. Ni katika maelezo haya alinieleza juu ya namba 666. Nilishangazwa sana na maelezo yake lakini nilipiga moyo konde nikiamini tiba ipo.
Baadaye akanieleza jinsi alivyojitoa katika harakati hizo za kumtumikia shetani. Haikuwa njia rahisi. Aliwapoteza ndugu zake kadhaa lakini mwisho akawa amejikomboa.
Hiyo chapa uliyopigwa lazima ifutwe! Ni njia hiyo tu ya kukukomboa kutoka ufalme huo.
Nilikuwa makini nikimsikiliza.!

***R.I.P jina jipya katika simulizi…mbwembwe za kutosha….je atamsaidia ISABELA kuibandua ile chapa ya 666…….
ROHO ILIYO POTEA……
**Kama unahitaji kupata simulizi hii mwanzo mwisho katika inbox yako, wasiliana na mtunzi 0654 960040…..
ITAENDELEA KESHO!!!!

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top