Unknown Unknown Author
Title: TAMBWE HIZA ABOMOA NGOME YA CUF JIMBO LA MCHINGA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
WANACHAMA wa chama cha mapinduzi Kata ya mipingo Kijiji cha Matapwa wilaya Lindi Jimbo la mchinga wakicheza kwa furaha baada kuwapokea wanac...

E82A1283WANACHAMA wa chama cha mapinduzi Kata ya mipingo Kijiji cha Matapwa wilaya Lindi Jimbo la mchinga wakicheza kwa furaha baada kuwapokea wanachama zaidi ya 120 waliohama chama cha wananchi
cuf na kujiunga na chama hicho tukio limesababisha tawi la chama cha
wananchi kubaki na mwenyekiti na katibu wake
E82A1003Mwenyekiti wa ccm mkoa wa Lindi Alli Mohamed Mtopa akimkabidhi kadi ya CCM Fatuma hamisi mkazi wa kijiji cha Matapwa jimbo la mchinga aliyeyehama chama cha wananchi cuf na kujiunga na chama hichoE82A1059Mwenyekiti wa ccm mkoa wa Lindi Alli Mtopa akimkabidhi kadi ya CCM miongoni mwa wanachama 120 wa kijiji cha Matapwa jimbo la mchinga hadija Saidi aliyehama chama cha wananchi CUF na kujiunga na chama hicho

Na Abdulaziz video
WANACHAMA wa chama cha wananchi (Cuf ) tawi la Matapwa Jimbo la Mchinga wamekiama chama hicho na kuamia chama cha mapinduzi huku wakiliacha tawi ili likibaki na wanachama wawili akiwemo mwenyekiti na katibu yake,

Tukio hilo limetokea jana kwenye mkutano wa adhara uliitishwa na
mbunge wa jimbo la mchinga saidi mtanda wakati alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika jimbo.
Akizungumza kabla ya kugawa kadi kwa wanachama zaidi ya 120 wa tawi hilo lililokuwa ngome ya cuf katika jimbo Hilo la Mchinga kiongozi
mwandamizi wa chama cha mapinduzi taifa Tambwe Hiza aliwataka
wananchi wa kata hiyo kuachana na siasa za kichochezi zinazo
sababisha uvunjifu wa amani badala yake wafanye kazi za kujiletea
maendeleo yao.

Tambwe alisema hakuna chama kinachotawala duniani ambacho kinagawa fedha kwa wananchi wake kwa ajili ya kuendesha maisha yao ya kila siku bali ilani, na sera mzuri kama za ccm ndizo zinawafanya wananchi wao kuwa na maendeleo ikiwemo upataji wa huduma muhimu za kijamii kama vile. Maji, elimu, miundombinu pamoja na huduma za Afya.

Aidha Tambwe aliwaomba wananachi wa jimbo hilo ambao hawajajiunga na chama hicho kujiunga haraka na kuachana vyama vyenye itikadi za kibaguzi, kidini na kueleza kuwa chama Ccm ndicho chama pekee nchini chenye sera mzuri na mwelekeo wa kuwaletea maendeleo wananchi yake,

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top