STEVEN KANUMBA JR AZALIWA, MAMA KANUMBA, MAMA LULU NA LULU WAJAWA NA FURAHA.

Mama Lulu na Mama wa marehemu Steven Kanumba wanaonekana kuwa karibu sana siku hizi na hivyo watu kuzidi kuamini kuwa hawana tofauti tena na kusahau yaliyopita.Dada wa marehemu Steven Kanumba amejifungua hivi karibuni katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili na mtoto huyo kupewa jina la Steven Kanumba Jr huku mama mzazi wa Elizabeth Michael(Lulu) na mama Kanumba wakiwa na furaha sana,clip_image002Lulu pia alionyesha furaha yake kwa kuzaliwa mtoto huyo kama picha zinavyoonekana hapo.

Tunawapongeza tena na tena wazazi hao kwa kuwadhihirishia wanajamii kwa mara nyingine kuwa kila mtu ana amani na mwenzake na hakuna tofauti yoyote kati yao. Mtoto huyo amepewa jina la Kanumba kama ishara ya kumuenzi muigizaji Steven Kanumba aliyekuwa maarufu Afrika mashariki na kuanza kujulikana kimataifa.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post