NIGERIA YABAKI KUWA TIMU PEKEE KUTOFUNGWA KWENYE KOMBE LA MABARA TANGU KUANZISHWA KWAKE BAADA YA KUIPA KIPIGO CHA 6-1 TAHITI
Timu ya taifa ya Nigeria tarehe 17/06/2013 iliitandika TAHITI mabao 6-1 kwenye michuano ya kombe la mabara inayoendelea huko nchini Brazil. Mchezo huo umetengeneza takwimu nyingi sana - zipo kama ifuatavyo:
- Nnamdi Oduamadi ndie mwanasoka wa kwanza wa kiafrika kufunga mabao 3 kwenye mechi moja katika michuano ya Mabara
- Jonathan Tehau ndio mchezaji wa kwanza wa Tahiti kufunga goli kwenye michuano ya FIFA
- Nigeria wanabaki kuwa ndio timu pekee ambayo haijawahi kupoteza mchezo katika historia michuano hii kwa timu ambazo zimewahi kushiriki. Wakishinda mara mbili na kutoa suluhu mara mbili.
- Jonathan Tehau ndio mchezaji wa kwanza kufunga kwa pande zote kwenye mechi ya michuano ya FIFA - na bado timuyake ikafungwa. Wachezaji sita wengine waliowahi kufanya hivyo wote timu zao walizokuwa wakizichezea zilishinda mechi zao.
- Matokeo ya Tahiti 1-6 Nigeria ni matokeo ya moja kati ya mechi 8 za kombe la mabara zilizozaa magoli mengi - 7. Ni mechi moja tu ya Brazil 8-2 Saudi Arabia ndio imezidi idadi hiyo ya mabao kwa mechi.
Habari kwa hisani ya Shaffihdauda