Unknown Unknown Author
Title: MKUU WA MKOA WA LINDI AZINDUA KAMPENI YA MAMA MISITU WILAYANI NACHINGWEA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Ludovick Mwananzila akipanda mti kuashiria Uzinduzi wa Kampeni ya Mama Misitu wilayani Nachingwea Mkunzi mtendaji wa H...

IMG_0809Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Ludovick Mwananzila akipanda mti kuashiria Uzinduzi wa Kampeni ya Mama Misitu wilayani NachingweaIMG_0831Mkunzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea,Valery Kwembe ambae amehamia Wilaya hiyo siku mbili zilizopita akitokea wilaya ya Mpanda nae akipanda Mti ikiwa ishara ya kupokea mradi huo Wilayani kwakeIMG_0973Bango la mama misituIMG_1031Meneja kampeni Kitaifa mpango wa MAMA MISITU,Gwamaka
Mwakyanjala akitoa maelezo mafupi ya kampeni hiyo kwa mkuu wa mkoa wa lindi katika uzinduzi huo
IMG_0920Watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Nachingwea waliohudhuriaIMG_0994Wananchi mbalimbali waliohudhuriaIMG_1001Mkurugenzi wa mradi wa Mpingo,Gasper Makala akisoma taarifa fupi ya Uzinduzi wa MAMA MISITU

Na Abdulaziz Video,Nachingwea
Wananchi Mkoani Lindi wametakiwa kutunza na kuhifadhi Misitu ya Vijiji ikiwa pamoja na kudhibiti Uchomaji moto ovyo wakiwemo wavunaji haramu ili misitu hiyo inufaishe jamii husika.

Wito huo umetolewa leo na Mkuu wa mkoa wa Lindi Ludovick Mwananzila alipokuwa akizindua program ya kuelimisha jamii pamoja na kuwahamasisha juu ya faida za misitu na kutetea zaidi Udhibiti wa
Misitu Nchini(MAMA MISITU)Uzinduzi ulioenda sambamba na Siku ya
Mazingira duniani iliyofanyika kimkoa katika kata ya Ruponda Wilayani Nachingwea.

Kufuatia mpango huo wa Mama Misitu jamii/Wanachama wa mtandao watapewa nafasi ya kuainisha na kujipangia shughuli za ufuatiliaji katika hatua za utekelezaji wa taratibu za uvunaji ikiwa pamoja na utekelezaji wa Sheria Muhimu za Misitu

Ufuatiliaji wa jamii utaongeza tija na uelewa kwenu katika kujua thamani ya misitu yenu leo nazindua mpango huu wa Mama Misitu kazi kwenu najua kamati za uvunaji zipo,za ulinzi zipo na Serikali aitawafumbia macho wanaohujumu Misitu’alimalizia Mwananzila

Awali Mkurugenzi wa Mradi wa Uhifadhi wa Mpingo,Gasper Makala akisoma taarifa fupi ya uzinduzi huo aliomba ushirikiano katika usimamizi bora wa Misitu kati ya Taasisi za Serikali, Taasisi binafsi na jamii wanaojishughulisha na matumizi ya mazao ya misitu kuhakikisha kunakuwa na usimamizi endelevu wa rasilimali ya misitu

Uzinduzi huo katika wilaya ya Nachingwea pia uliambatana na Burdani
mbalimbali ikiwemo Upandaji Miti Ulioongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi sambamba na kukabidhi Cheti na Zawadi kwa kijiji cha Ruponda kwa Uhifadhi bora na utunzaji wa Mazingira

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top