MFULULIZO WA VIFO VYA WASANII WAMFANYA DOKII AFUNGUKE KUWA NI MUNGU ANAWAADHIBU

clip_image001MWIGIZAJI Bongo, Ummy Wenslaus ‘Dokii’ ameibuka na kusema kuwa vifo vya wasanii vimetokea kutokana na kujisahau hivyo Mungu ameamua kuwaadhibu.
Akiongea na mwandishi wetu katika Viwanja vya Leaders Club, Juni 5, mwaka huu ambapo mwili wa Mangwea ulikuwa ukiagwa, Dokii alisema matukio ya vifo vya wasanii mbalimbali yaliyotokea miaka miwili mfululizo ni pigo kubwa kwani wengi ni vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa kitu ambacho anakiona ni ishara kuwa Mungu anataka kujidhihirisha kwa wasanii.

“Wasanii tulijisahau sana na kuona Mungu hayupo kwani kipindi bado hatujatoka na tunatafuta kutoka kisanaa, tulikuwa tunamuomba kila wakati lakini baada ya kutoka na kuwa mastaa tumemsahau kabisa.
“Hatukumbuki kwenda ibadani tunabaki kuendekeza starehe za dunia tu, hivyo tubadilike kwani Mungu ameanza kujionesha kwetu kwamba yupo,”
alisema Dokii.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post