Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF, Absalom Kibanda) amewasili hivi punde katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere nchini Tanzania, na kumwaga chozi akitokea Afrika Kusini alikokwenda kwa matibabu baada ya kutekwa na kuteswa na watu wasiojulikana.
Akizungumza na waandishi wa habari hivi punde, Kibanda ameshukuru vyombo vya habari kwa mshikamono na ushirikiano alioupata tangu siku ya kwanza alipokubwa na mkasa huo.
Vile vile ameshukuru watu wengine mbalimbali waliojitokeza kumsaidia kwa namna yoyote ile.
Pia amelishukuru jukwaa la wahariri na vyombo vingine vya habari jinsi walivyoripoti baada ya kutekwa na kuteswa mpaka kuhamishiwa katika hospitali Afrika Kusini.
"Tukio hili linafafana na lile la Ulimboka. Nawaombea waandishi wenzangu msipate maumivu niliopata mimi," amesema.
Pia amesema kwamba Mwenyezi Mungu akimpa uzima atalizungumzia tukio la kutekwa na kuteswa siku nyingine.
Baada ya Absalom Kibanda kuwasili wa Uwanja wa Ndege ameonekana akilia kutokana na waandishi wenzake waliomiminika kwa wingi kumpokea pamoja na watu wengine huku waandishi wa habari wakijitahidi kupata picha yake. Mpaka habari hii inarushwa katika habarimasai.com bado Kibanda alikuwa akiendelea kulia.
Amesema akiwa Afrika ya Kusini mwenyeji wake alikuwa ni Fredy Masika ambaye ni kiongozi wa Jumuiya ya Watanzania nchini humo.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.