Zile show zilizokuwa gumzo takribani wiki tatu hapa tz zimefanyika jana na kuhudhuliwa na mashabiki lukuki kwa kila mtu kuchagua wapi angeweza kwenda kupata kile alichotarajia kukipata toka kwa msanii ampendae kati ya hawa wawili nikimaanisha Show ya Miaka 13 ya Lady Jaydee na The finest ya Mwana FA.
Tuanze kuangalia muonekano wa Wasanii hawa nadhani kila msanii alijiandaa kutokelezea kulingana na Show yake jinsi ilivyokuwa hapa nikimaanisha maudhui ya show hiyo, Sasa hebu tuambie ni nani ametokelezea kuliko mwenzake?Pia wawapo stejini lazima uitumie vizuri jukwaa hilo ili kukonga nyoyo za mashabiki wako waliokuja kuhudhulia show ili uwape haki yao ya kile walicholipia kuja kukiangalia sasa hebu tuambie ni nani aliwashika Mashabiki wake kati ya Lady Jaydee na Mwana FA….