EDIBILY LUNYAMILA, MOHAMED HUSSEIN MMACHINGA WARUDI DIMBANI

clip_image001Timu ya wachezaji wakongwe waliowahi kutikisa katika soka la Tanzania - Wakongwe FC wameunda timu ambayo imeingia kwenye kombe la mchangani linaloitwa Beira Cup linalofanyika viwanja vya Beira maeneo ya Kigogo hapa jijin dar es salaam.
Timu hiyo inaundwa na wachezaji wengi wa zamani kama vile Mtwa Kihwelu, Jemedari Said Kazumali mshambuliaji wa zamani wa kariakoo ya lindi, 82 Rangers ya Shinyanga na JKT Ruvu ambaye kwa sasa ni meneja Azam, kiungo wa zamani wa Ushirika ya Moshi na Yanga Steven Nyenge, winga wa zamani wa biashara ya Shinyanga, Yanga, Simba na Malindi Edibily Lunyamila, mshambuliaji wa zamani wa Bandari ya Mtwara, Yanga na Simba Mohamed Hussein 'Mmachinga', kiungo wa zamani wa Simba George Lucas "Gazza", Ally Yusuf 'Tigana', Ngade Chabanga, Bakari Idd, Benny Mwalala, mshambuliaji wa zamani wa Cosmopolitan ya jijini Dar Shaffih Dauda, kiungo wa zamani wa Miembeni ya Zanzibar Ibrahim Masoud 'maestro' na wengineo kibao
Timu hii ya Wakongwe FC jana ilicheza mechi yake ya kwanza na kuifunga Young Kids ya Tabata kwa bao 1-0 - goli lilofungwa na Ben Mwalala.Shaffih Dauda na Lunyamila

SOURCE: SHAFFIHDAUDA

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post