Unknown Unknown Author
Title: WAZO HURU: MACHAFUKO NCHINI, “VURUGU ZA KIDINI ZINA MKONO WA WATU NCHI ZA NJE”
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na: Ochu Kunambi, Lindi Gesi, mafuta na madini maalum ya kutengeneza nishati ya nyuklia au Uranium ndivyo vitu vinavyolitoa udenda taifa f...

901164_10151369400865793_1541535301_o

Na: Ochu Kunambi, Lindi

Gesi, mafuta na madini maalum ya kutengeneza nishati ya nyuklia au Uranium ndivyo vitu vinavyolitoa udenda taifa fulani kubwa kiuchumi duniani hadi kujaribu kuiingiza Tanzania katika vita ya udini.. Walijaribu kutugombanisha na jirani zetu Congo, kwa kusema sisi ndio tunawasapoti waasi kwa kuwapa silaha, wakashindwa. Wakajaribu kutugombanisha na Malawi, tena wakidiriki kusema Ziwa Nyasa ni la Malawi katika vyombo vyao vya habari kana kwamba wao ndio mahakimu. Yote hiyo haina nguvu kwa kuwa ugomvi wa ndani/nje ni rahisi kuisha na kutatulika isipokuwa wa ndani kwa ndani, ni ngumu. Rejea mifano ya Rwanda, Burundi, Somalia, Congo DRC n.k. jinsi zilivyochukua muda kurudi angalau ktk utulivu. Ni miaka mingapi imepita ilhali bado makovu yanajionyesha dhahiri au bado wanahaha kuisaka amani iliyotoweka? Sasa wamekuja na njia thabiti ya kutugawa ndani kwa ndani kwa msingi wa udini. Hiyo ina nguvu na inaweza kutugawa kweli niwe mkweli hapa, kwa kuwa ndani huathiri nje kirahisi na kwa haraka na kinyume chake si muhimu. Wangeweza kutumia njia ya ukabila kutugawa kwa ndani ila wameona haiwezekani, tuko imara. Ndio maana wameamua kutumia penye ufa au pale penye udhaifu. Upekuzi nilioufanya nimeona hata kupeleka mashushushu kuchunguza mauaji ya Padri na hata milipuko iliyotokea Arusha juzijuzi pia ni sehemu ya sera zao na mikakati ya kumomonyoa mshikamano na kuchochea mgawanyo. Tuna uhakika gani kuwa hawako nyuma ya mauaji hayo? Tafakari kwa kina ukijiweka ktk upande huria (neutral) utapata maswali mengi ya kujiuliza ktk hili. Na kauli ya Rais Kikwete kuwa, "vurugu za kidini zina mkono wa watu wa nchi za nje" ya juzi juzi kwenye ibada ya Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana si ya kubeza. Mimi nimemuelewa zaidi ya aliyoweka bayana. Tufanye nini sasa? Chukua tahadhari Mtanzania mwenzangu. Hawa jamaa wako smart kucheza na akili za watu pindi watakapo kitu, bila kujali umwagikaji wa damu. Ukielewa haya hutatingishwa na mtu yeyote asiyelitakia mema taifa lako. Umoja wa kitaifa ni muhimu kwa maendeleo ya taifa lolote.

https://www.facebook.com/ochu.kunambi?hc_location=stream

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top