UPDATES KIFO MANGWEA: M2 THE P ADAIWA KUWA YUPO HAI ILA YUPO ICU

clip_image001Taarifa zilizotufikia hivi punde kutoka nchini Afrika Kusini ni kwamba yule msanii aliyepelekwa hospitali pamoja na Mwana Hip Hop, Albert Mangwair aitwaye M to the P bado hajafa bali yupo ICU akiendelea na matibabu. Hapo mwanzo tuliripoti kuwa ameshafariki kutokana na kupokea taarifa kupitia akaunti ya mtu wa karibu kabisa alioko huko kuripoti kifo chake

Msilikize Daktari akithibitisha

M2 the P alipelekwa katika hospitali ya St. Hellen iliyopo nchini humo kwa matibabu baada ya kukutwa amepoteza fahamu akiwa na Mangwair aliyefariki dunia jana. Mwili wa marehemu Mangwair bado upo katika hospitali ya St. Hellen na mipango ya kuhamisha mwili huo bado inaendelea. Baadhi ya Watanzania waishio nchini Afrika Kusini wamejikusanya kwa ajili ya kuandaa mipango ya kuhifadhi mwili huo pamoja na safari ya kuuleta nchini Tanzania.clip_image001[6]Marehemu Albert Mangwair akiwa na mshikaji Hamisi, Jumamosi hii siku ya Fainali ya UEFA kati ya Bayern Munich na Borusia Dortmund. Ngwair alishabikia

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post