Produza wa Mj Records Marco Chali akiwa kwenye interview pamoja na Godzila akizungumzia 'Marco Chali' Foundation itakayozinduliwa Mwembe Chai siku ya tarehe 26.
Kwa kushirikiana na Zantel Marco Chali atazindua Foundation yake ambayo lengo lake ni kutoa mafunzo kwa vijana kuhusu muziki, na pia baadae kuwasaidia wasanii wenye vipaji vya kufanya muziki kutimiza ndoto zao.Tamasha hilo linaend kwa jina la Epic Open Mic litakuwa msaada kwa watu wote wenye ndoto zakuja kuwa msanii mkubwa.Pamoja na uzinduzi wa Marco Chali Foundation wasanii wakali ambao Marco Chali amewahi kuwatengenezea nyimbo wataperform kama Madee anayefanya vizuri na wimbo wa 'Pombe Yangu',Godzila anayefanya vizuri na 'Nataka' aliyoshirikiana na Marco Chali,Daimond, Mshindi wa EBSS Walter Chilambo,Slim Sal,Ney wa Mitego,King Kapita na wengine kibao.
Tags
HABARI ZA WASANII