TANZIA: BIBI KIDUDE AFARIKI LEO HII..!!!

BREAKING NEWS:
557964_566928410006701_245831023_nBi Kidude amefariki dunia mapema leo mjini Zanzibar. mara kadhaa Bi kidude, ambaye amejipatia sifa na umaarufu ndani na nje ya nchi, amekuwa akizushiwa kifo kutokana na kuuguawa muda mrefu....
Mwili wa Bi Kidude utahamishiwa kwake Rahaleo na mazishi yatakuwa kesho. 

Bi Kidude alizaliwa katika kijiji cha Mfagimaringo, alikuwa binti wa mchuuzi wa nazi, hakuna anayejua haswa Bibi huyu alizaliwa tarehe ngapi, kuna hata mawazo kuwa alikwishafikisha miaka 102. 

Katika mwaka 1920 tayari alikuwa amekwisha anza kuimba katika vikundi vya sanaa kule kwao, mwaka 1930 alijiunga na Egyptian Musical Club ya Dar es Salaam na kuzunguka miji mingi ya Tanganyika wakati ule , mwaka 1940 alirudi Zanzibar ambako awali alikuwa amekimbia kwa kuwa aliozwa kwa nguvu na mtu aliyemzidi sana umri.

Bi Kidude pia liwahi kuimba na Sitti Binti Sadi wakati wa ujana wake, na katika maisha yake Bi Kidude amekwisha zunguka mabara yote akiimba katika majukwaa na wanamuziki maarufu ulimwenguni


 Timu nzima ya Blog ya LINDI YETU  ina toa pole kwa familia, ndugu jamaa na marfiki na TAIFA kwa kufikwa na msiba huu

MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI--AMIN!

 AMESHAZUSHIWA KIFO MARA KADHAA...
Usiku wa kuamkia October 26, 2011 ujumbe ulisambazwa kwenye mitandao ya simu za mkononi na mitandao ya kijamii, Facebook na Twitter kuwa Bi Kidude amefariki dunia! Moja ya SMS hiyo ilisomeka: Qaallu Inna Lillahi Wainna Ilaihi Raajiuni; BI KIDUDE AMEFARIKI DUNIA! Habari ambazo zimekanushwa vikali na mwenyewe siku hiyo asubuhi. Kudhidirisha kweli hajafa, Bi. Kidude aliongea moja kwa moja na Radio One na kumwambia mtangazaji aliyetaka kujua ukweli wa habari hizo kwa kumjibu: "Maiti haiongei, mimi ndiye Bi Kidude, mzimaaa!" HII NI TABIA AMBAYO INAKUWA KWA KAZI YA KUZUSHIA WATU VIFO KWA KUTUMIA MITANDAO YA SIMU NA KIJAMII


MAISHA ALIYOISHI BI KIDUDE ENZI ZA UHAI WAKE
Maskini Bi Kidude! Ndiyo kauli pekee inayoweza kukuponyoka kinywani ukimtembelea Mwanamuziki mkongwe wa Taarab Bongo, Fatuma Binti Baraka ‘Bi Kidude’, Risasi Mchanganyiko limemshuhudia.
Maisha ya mkongwe huyo aliyeanza muziki mwaka 1920 akiwa na miaka 13, yanasikitisha (hohehahe) kutokana na kutokuwa na hadhi ya jina lake linalotambulika ndani na nje ya Bongo.

The 5 Star Paper, Risasi Mchanganyiko, mwishoni mwa wiki iliyopita lilitia maguu nyumbani kwake maeneo ya Raha Leo, Zanzibar na kushuhudia maisha magumu anayoishi staa huyo ambaye kwa sasa anakadiriwa kuwa na miaka 104.

Kwa mujibu wa Bi Kidude aliyezaliwa maeneo ya Mferejimaringo, Zanzibar, nyumba anayoishi imezeeka na haijamalizika kujengwa na hata kupakwa rangi kiasi ambacho mvua ikinyesha lazima alowe kama hataweza kukimbilia upande mwingine kutokana na kukosa kipato cha kuikamilisha.

Katika mahojiano yake na mwandishi wetu, staa huyo alifanya kazi ya kujitolea ya muziki kwa zaidi ya miaka 90 alisema, hakuna mtu asiyejua maisha magumu anayoishi kwani hata Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete anamfahamu vilivyo hivyo hana haja ya kujieleza zaidi kwa kuwa kila kitu kinaonekana kwa macho yasiyohitaji miwani.

Mkongwe huyo ambaye ni nembo halisi ya utamaduni wa Mtanzania alisema:
“Siwezi kusema chochote juu ya maisha yangu mabaya kwani nitawaliza watu.

“Mtu yeyote ayatazame maisha yangu aone anachoweza kunifanyia kwani niliweza kuitangaza Jamhuri (Tanzania) vyema kwa maana hakuna nchi ambayo sijawahi kuitembelea kwa ajili ya kueneza utamaduni wetu.”



BAADHI YA SHOW ALIZOWAHI KUFANYA JIJINI DAR ES SALAAM. HII ILIKUWA June 30, 2012
                                                                Bi Kidude akiimba
Shabiki akimtunza Bi Kidude
Mashabiki wakipozi juu ya jukwaa ili kupiga picha na Bi Kidude.
Bi Kidude akionyesha umahili wake wa kucheza.
Hii ilikuwa usiku wa june 30 2011 katika ukumbi wa Equator uliopo Mtoni kwa Azizi Ally ambapo kulifanyika onyesho la taarab, wanamuziki mbalimbali wa taarabu waliudhuria akiwemo mwanamuziki mwalikwa toka Zanzibar Bi Kidude.
Baadhi ya bendi ambazo ziliudhuria onyesho hilo ni Five Star, TOT, East Africa Melod na Mashauzi Clasc

Baadhi ya picha enzi za uhai wake
Akitaniana na mtangazaji wa Clouds Tv, Sakina Lyoka
Akipiga ngoma
INNA LILAHI WAINNA ILAIHI RAAJIUUN.
Previous Post Next Post