Sharifu Maloya-Mratibu wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Lindi akifanya uhamasishaji kwa Wananchi wa kijiji cha Mandawa wilayani ili wajiunge na Mfuko wa Afya ya Jamii...
NHIF kesho katika hospital ya Sokoine Lindi.
Uzinduzi wa huduma hiZi utafanywa rasmi siku ya jumatatu(KESHO) tarehe 8.4.2013,Mgeni rasmi ni mkuu wa mkoa wa Lindi pia uzinduzi huo utahudhuriwa na Mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,Ndg Emmanuel Humba.
Akitoa taarifa hiyo kwa Waandishi wa Habari,Meneja wa ofisi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Lindi,Bi Fortunata Kullaya alieleza kuwa
hatua hiyo imekuja ili kusaidia huduma kwa wateja wa Mfuko huo na
wagonjwa wengine ambapo wagonjwa wasio wateja wa Mfuko watatumia taratibu za kawaida zilizopo katika kupata matibabu
Hivi karibuni Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Kwa kushirikia na Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA)Imetoa mafunzo kwa vikundi mbalimbali vya wajasiliamali katika wilaya za Lindi na Kilwa ili wajiunge na mfuko wa Afya ya Jamii(CHF) NA Kutoa msaada wa Mashuka kwa Hospital za Wilaya ya Ruangwa na Kilwa.