MAJI YAPUNGUA CHIPITE NA HALI YA USAFIRI KATIKA WILAYA ZA MIKOA YA LINDI NA MTWARA YAREJEA

MAMBO (2)Hali halisi ilivyo kuwa katika eneo la Chipite,MAMBO (1)

Na: Abdulaziz Lindi

Baada ya Maji kupungua katika eneo la Chipite ambalo lilijaa maji na

kusababisha Abiria zaidi ya 500 na Magari zaidi ya 200 kushindwa

kupita eneo na Kufanya gari nyingi ziendazo na Kutoka Mtwara, Masasi, Ruangwa, Liwale, Nachingwea, Liwale, Nanyumbu na Tunduru kufanya safari kwa kuzunguka wilaya ya Newala sasa hali imeanza kubadilika na gari nyingi kuanzia jioni zimeanza kupita ingawa kwa Mashakamashaka ili kusaidia kupeleka na kutoa huduma kwa Jamii Kufuatia hali hiyo baadhi ya wasafiri waliokwama wametupia lawama kwa Wakala wa Barabara Tanroads na Kitengo cha Maafa kutotoa Ushiriakiano wowote kuhakikisha Abiria wanakuwa kwa usalama ikiwa pamoja na kutafuta jitihada za haraka kuwavusha ili kuepusha Maafa yatakayochangiwa na uwepo wa msongamano kwa muda mrefu.

Hali ya usafiri sasa iko kama kawaida kuelekea katika wilaya Tajwa hapo Juu.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post