Na: Fungwa K, Lindi
Ikiwa ni Mechi ya Pili katika Ligi daraja la tatu iliyoanza mjini Lindi hapo Jana, leo hii ilizikutanisha Timu Mbili ambazo zinawashabiki wengi mjini hapa ambazo ni Kariakoo Fc na Marketi Fc, Kipindi Cha kwanza Timu ya Kariakoo Fc ndiyo iliyokuwa ya kwanza kufungua milango ya Magoli kwa kupitia Mchezaji wao Anafi kuifungia timu yake goli la kwanza kwa mkwaju wa penati.
Hata hivyo waliweza kuendelea kuonesha Soka safi kwa kupiga pasi za uhakika na cotrol za hali ya juu ambazo ziliwafanya mashabiki wao kushangilia muda wote wa mchezo, Dakika ya 22 ya mchezo Kariakoo walipata goli la pili ambalo liliwekwa kimiani na Nasoro Yahaya goli lapili liliwafanya Wachezaji wa Market Fc wazinduke na kujaribu kubadilisha mchezo na kuweza kuwazuia vizuri wapinzani wao na waliweza kupata goli la kwanza kwa upande wao mnamo dakika ya 34 kwa kupitia mchezaji Kakacho Hadi kipindi cha Kwanza kina malizika Kariakoo FC walikuwa mbele (2 – 1).
Kipindi cha pili kilianza kwa Timu zote mbili kushambuliana kwa zamu na Dakika ya 8 Kariakoo Fc waliweza kupata goli la tatu kwa kupitia tena mchezaji wao Selemani Mkonde, Kariakoo Fc Waliendelea kuonesha kandanda safi ambalo liliwalazimisha wachezaji wa Market Fc kucheza Rafu kila wakati na refalii kuwa zawadia kadi kadhaa za manjano. dakika ya 28 ya kipindi cha pili Kariakoo Fc waliweza kufunga ukurasa wa magoli baada ya mchezaji Nassoro Yahaya kupiga kichwa mpira uliopigwa klosi na kuweza kumpita golikipa na kutinga wavuni hili likiwa ni goli lake la pili katika mchezo huo. Hivyo Hadi kufikia mwisho wa Mchezo Kariakoo FC wakitoka kifuambele kwa magoli 4 dhidi ya Market Fc 1.
ANGALIA BAADHI YA MATUKIO KATIKA PICHA
Wachezaji wa Marketi Fc wakienda mapumziko, Hapa wakijadiliana juu ya kuwadhibiti wapinzani wao Kariakoo Fc. ( 4 – 1)
Refaree wa Leo MIKAPA huyoo akijongea kwenye chumba cha mapumziko Uwanja wa Ilulu Mjini Lindi. (Kariakoo Fc 4 Market fc 1)
Mashabiki wa Kariakoo Fc wakiangalia kwa makini jinsi mchezo ulivyokuwa ukichezwa leo uwanja wa Ilulu (Kariakoo Fc 4 Marketi Fc 1)
Mashabiki wa Market Fc wakiwa kimya kabisa wakiangalia jinsi timu yao ilivyokuwa ikinyanyaswa kwa soka safi toka kwa wapinzani wao (Kariakoo Fc 4 Marketi Fc 1)
Wachezaji wa kariakoo Fc wakishangilia Ushindi wao wa Goli La Nne (Kariakoo Fc 4 marketi Fc 1)
Wachezaji wa kariakoo Fc wakishangilia Ushindi wao wa Goli La Nne (Kariakoo Fc 4 marketi Fc 1)
Tags
SPORTS NEWS