MTANGAZAJI wa Kipindi cha Wanawake Live kinachorushwa na Runinga ya EATV ya jijini Dar, Joyce Kiria amejianika nyumbani kwake akimnyonyesha mwanaye wa pili wa kiume aitwaye Linston. Kwa mujibu wa picha iliyowekwa na mtangazaji huyo katika mtandao wake, inamuonesha akiwa amekaa katika kochi nyumbani kwake Kinondoni jijini Dar akimnyonyesha mwanaye huku akichombeza kwa maneno; ‘Mwanamke kunyonyesha, chezeya. Sasa hivi kono kono... misupu, mitori kwa wingi ili mtoto apate maziwa ya ukwee...chezeyaa.’ Linston ni mtoto wa pili wa Kiria ambaye alifunga ndoa na Henry Kileo mwaka 2011, mtoto wa kwanza aliyezaliwa mwaka jana anaitwa Lincon.
![clip_image002[5] clip_image002[5]](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjWiQr5ltDcQKKmU42Z1KWZIMF8fGQsvoJIqskUbkuha1YT0ZtVJ7Vl9Hez8APmSRc12GjyngeE6BDV7L46nT40OfsylpbVe0Os86dN09dS8dLYTnVc9MkY4f0VbvHwF25LBGsKaAyUDug/?imgmax=800)