Vodacom Foundation yasaidia vifaa vya hedhi shule za msingi


Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,wakifurahia jambo pamoja na wanafunzi wa shule za msingi  Barazani  na Qambasirong zilizoko mkoani manyara,wakati walipofanya ziara ya kutembelea shule hizo na kutoa msaada wa pedi za kisasa zinazofuliwa na zenye uwezo wa kudumu kwa mwaka mmoja pamoja na nguo za ndani vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni saba.Meneja Idara ya wateja wakubwa wa Vodacom Tanzania Bi.Stela Mamuya akigawa msaada wa pedi za kisasa zinazofuliwa na zenye uwezo wa kudumu kwa mwaka mmoja pamoja na nguo za ndani kwa wanafunzi wakike wa  shule za msingi Barazani  na Qambasirong zilizoko Haydom wilayani Mbulu mkoani Manyara,msaada huo uliotolewa na Vodacom Foundation umegharimu zaidi ya shilingi Milioni saba.
Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Barazani, Haydom mkoani Manyara,Bi.Magreth Shirima wapili toka kushoto akielekezwa na mfanyakazi wa Vodacom kitengo cha huduma kwa wateja Bw.Ndaro Laban kulia na Esther Mattle namna bora ya matumizi ya pedi za kisasa zinazofuliwa na zenye uwezo wa kudumu kwa mwaka mmoja zilizotolewa na Vodacom Foundation kama msaada kwa wanafunzi wa shule za msingi  Barazani  na Qambasirong zilizoko mkoani humo,thamani ya vifaa hivyo vimegharimu zaidi ya  shilingi milioni saba.Mfanyakazi wa Idara ya wateja wakubwa wa Vodacom Tanzania,Bw.Simon Martin akimkabidhi pedi za kisasa zinazofuliwa na zenye uwezo wa kudumu kwa mwaka mmoja pamoja na nguo za ndani mwanafunzi wa kidato cha sita Bi.Getrude Boniphace, zilizotolewa na Vodacom Foundation kama msaada kwa wanafunzi wa shule za msingi  Barazani  na Qambasirong zilizoko mkoani manyara,thamani ya vifaa hivyo vimegharimu zaidi ya  shilingi milioni saba,anaeshuhudia katikati ni Mkuu wa kitengo cha msaada kwa wateja wakubwa Bw.Ally Zuber.
Previous Post Next Post