Awali tulitoa habari za mtoto huyu akiomba msaada lakini hadi sasa bado hajapata msaada wowote ule wa kuweza kuokoa maisha yake. Nahivi sasa hali ya mtoto huyu inazidi kuwa mbaya kiafya .
Mtoto Simon Mrope alikubwa na ugonjwa huo wa moyo tangu mwaka 2001 mara baada ya kuzaliwa na kugundulika kuwa moyo wake una tundu hali ambayo inamsababishia mtoto huyo kuvuta pumzi kwa shida.
Mama wa mtoto Simon Mrope anayeitwa AMINA ALLY anawaomba watanzania kumsaidia mtoto wake fedha za matibabu Baada ya kuambiwa na madaktari kuwa Simon anatakiwa kwenda nchini india kutibiwa,baada ya kupata rufaa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili mwaka 2006 huku familia yake ikiwa haina uwezo kabisa.
Majirani wa familia ya Simon nao wanasema kuwa mtoto huyo anahitaji msaada wa haraka kwa kuwa hali yake sio nzuri na kuwaomba watanzania wamsaidie.
Kinachosikitisha zaidi baba wa mtoto huyo anayejulikana kwa jina la MROPE ameondoka nyumbani hapo tangu mwaka 2011 na hajulikani aliko kwa sasa, ingawa mwanzoni alisema yuko nchini Msumbiji.
Kwa anayeguswa na tatizo hili na anataka kumsaidia SIMONI MROPE atumie simu namba +255752732290
Tags
HABARI ZA KITAIFA