Matukio punde yanapojiri:Uchaguzi Kenya

482363_400757246687547_1164096955_nHii leo wakenya wanapiga kura katika uchaguzi wa kihistoria chini ya katiba mpya. Foleni tayari zimeanza kushuhudiwa katika vituo.
Kinyang'anyiro ni kikali kati ya Muungano wa Cord na Jubilee wa Raila Odinga na Uhuru Kenyatta.
Kwenye ukurasa huu tutakupasha matukio kila yanapojiri hadi upigaji kura utakapokamilika mwendo wa saa kumi na moja jioni.
Unaweza kututumia maoni yako kuhusu uchaguzi kwenye ukurasa wetu wa facebook


18:22: Mwandishi wa BBC Jamuhuri Mwavyombo amesema kuwa kulika na matatu tofauti, mjini Mombasa ambako kundi la MRC linaendesha harakati zake. Mashambulio  mawili, yalifanyika mtaa wa Changamwe, ambako polisi walishambuliwa na tukio la tatu katika kituo cha polisi eneo la Chumani Kilifi.
16:27 :Sehemu nyingi za starehe na ulevi mjini Nyeri Mkoa wa Kati zimefungwa na zitafunguliwa Jumanne ili kuwaruhusu wapiga kura kupiga kura. Eneo la Mkoa wa Kati lina tatizo la uraibu wa pombe
16:24: Ng'endo Angela ambaye yuko Mkoa wa Kati anasema kuwa kuwa sababu ya hitilafu za kimitambo, tume imelazimika kutumia mfumo wa kawaida kwa kutumia daftari za wapiga kura. Ni Nyeri peke yake ambako shughuli hiyo ilifanikiwa kwa njia ya Elktroniki
15:54 Mwandishi wa BBC Emmanuel Igunza anasema kuwa foleni mjini Nakuru zimeanza kupungua na huenda wapiga kura wakamaliza shughuli hiyo itimiapo saa kumi na moja jioni muda wa mwisho wa kupiga kura

15:16 Mmoja wa wagombea wakuu wa urais Uhuru Kenyatta ameelezea maskitiko yake kuhusu yaliyojiri Mombasa ambako washukiwa wa kundi la MRC waliwaua polisi na raia katika mashambulizi usiku wa kuamkia leo. Lengo lao lilikuwa kuvuruga shughuli ya uchaguzi


14:57 Mwandishi wa BBC mjini Kisumu Ann Mawathe anasema milolongo ya watu imepungua sana katika sehemu nyingi za mji huo ikizingatiwa kuwa asubuhi watu walikuwa wamejaa pomoni

14:51 Kuna taarifa kuwa magari ya Abiria yameanza kuongeza nauli ya magari kwa sababu ya upungufu wa magari hayo wakati wakenya wakiwa wamejitokeza kupiga kura


13:33 Tume ya uchaguzi imeagiza uachaguzi kurejelewa katika wodi tano kati ya zote 1'450 ambako mitambo ya tume hiyo ilikumbwa na hitilafu pamoja na makosa kwenye karatasi za kupigia kura

13:31 Katika baadhi ya vituo vya kupigia kura, ambako foleni ndefu zimeshuhudiwa, taarifa zinasema kuwa watu wanaonekana kukata tamaa na wameamua kurejea nyumbani kwani foleni hazisongi


13:24 Mwandishi wa BBC Wanyama wa Chebusire anaripoti kuwa gari la mbunge mmoja wa zamani limeteketezwa moto katika kaunti ya Kakamega na watu wanaoaminika kuwa wafuasi wa mpinzani wake.
11:25 Mkuu wa Polisi David Kimaiyo asema kuwa takriban wanachama 200 wa kundi la MRC au Mombasa Republican Council walivamia kituo cha polisi wa doria wakiwa wanaelekea kusambaratisha shughuli za kupiga kura. Inaarifiwa polisi wanne
Previous Post Next Post