Ifuatayo ni taarifa ya Jill Mcgivering ikisimuliwa na Wanyama wa Chebusiri.
Kuongezeka kwa visa vya wanawake kuondolewa mfuko wa uzazi, ni kutokana na ongezeko la kliniki na hospitali za kibinafsi katika miaka ya hivi karibuni. Zote hizo zinajaza pengo la mfumo duni wa serikali hususan katika maeneo ya vijijini.
Wanaharakati wanataka hospitali hizo kuchunguzwa na hata kuwekewa sheria za utenda kazi ili kuhakikisha kuwa haziwanyanyasi akina mama maskini.
Anaelezea kuwa kuna mbinu nyingi tu ambazo, mfuko wa uzazi unaweza kuondolewa bila upasuaji, na kwamba hiyo inapaswa kuwa tu njia ya mwisho katika matibabu yoyote.
Baada ya kuondoa mfuko wa uzazi huwa ni vigumu kuthibitisha kuwa operesheni hiyo haikuwa budi kufanywa.
Lakini jambo la kushangaza ni kuwa wasichana wadogo wanaondolewa mfuko huo baada ya madakrati kuwatisha kuwa watapata saratani ikiwa hautaondolewa.
Waziri wa ustawi wa vijijini Jairam Ramesh, anasema kuwa changamoto kubwa ni kuwa mfumo wa serikali umeporomoka na kwamba watu hulazimika kwenda katika hospitali za kibinfasi,
Anasema kuwa kwa hilo watu hulazimika kutumia pesa nyingi sana na hata kupata matibabu wasiyoyahitaji.
Tags
HABARI KIMATAIFA