Kocha Msaidizi wa Simba SC, Jamhuri Kihwelo akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mchezo wao wa kwanza wa Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Recreativo de Libolo ya Angola kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Jamhiri amesema wamejiandaa vema na wanaamini watashinda kesho, hivyo amewataka wapenzi wajitokeze kwa wingi kuishangilia timu kesho.
Kocha Mkuu wa SImba SC, Patrick Liewig akifafanua jambo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mechi ya kesho dhidi ya Libolo. Liewig amesema wameiandaa vema timu yao na iko tayari kwa kuipigania ushindi kesho.
Source: Bin zubery
Tags
SPORTS NEWS