KIUNGO wa kimataifa wa Yanga, Haruna Niyonzima 'Fabregas' amezidi kuiimarisha timu yake katika kilelele cha ligi kuu bara baada ya kuifungia bao la ushindi timu yake dhindi ya Azam Fc katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa.Licha ya Azam kuonekana na uchu mkubwa wa kutaka kuendeleza ubabe wao kwa Yanga kama walivyofanya kwenye mzunguko wa kwanza, walishindwa kufua dafu baada ya kukutana na ukuta madhubuti wa Yanga.
Kwa ushindi huo Yanga imefikisha pointi 39 huku Azam Fc ikibaki na pointi zake 36 na kuendelea kushika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi hiyo.
Baada ya mchezo huo kumalizika wachezaji wa Azam, walimzonga mwamuzi wa mchezo huo kwa kile walichodai kuonewa sakata lililookolewa na askari wa usalama kwa kuwaondoa waamuzi hao uwanjani wakiwa chini ya ulinzi mkali huku wakipondwa na chupa za mikojo. Kikosi cha Yanga SC leo kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Simon Msuva, Frank Domayo, Jerry Tegete/Didier Kavumbangu, Hamisi Kiiza/Said Bahanuzi na Haruna Niyonzima.
Azam FC; Mwadini Ally, Kipre Balou/Jabir Aziz, Waziri Salum, Joackins Atudo, David Mwantika, Ibrahim Mwaipopo, Salum Abubakar, John Bocco, Kipre Tchetche, Humphrey Mieno na Khamis Mcha ‘Vialli’/Seif Abdallah