MKUTANO WA SITA WA MENEJIMENTI YA SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA (NIC) WAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Ndg. Justine Mwandu akifungua mkutano wa Sita wa Mameneja wa shirika hilo katika hoteli ya Sea Scape iliyopo maeneo ya Mbezi, Dar es Salaam tarehe 3 Desemba 2012. Kushoto ni Mkurugenzi wa Bima za Maisha, Bi. Rose Lawa na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Bi. Anne Mbughuni. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Bima za Mali na Ajali, Ndg Ndugu Kura Kalema.Mkurugenzi Mtendaji Bw. Mwandu (kushoto) akiwakaribisha wajumbe katika mkutano. Anayesalimiana nae ni meneja wa bima tawi la Songea Ndugu Moses Senje akifuatiwa na meneja mwenzake tawi la Tanga Ndugu Romanus Hokororo na mwisho meneja wa Iringa Ndg Ally Mohammed.Wakurugenzi pamoja na Mameneja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mkutano.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post