Unknown Unknown Author
Title: MHESHIMIWA RAIS AFUNGUA MAHAKAMA YA MWANZO, RONDO.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwa katika picha ya pamoja na Mheshimiwa Rais katika Ufunguzi wa Mahakama hiyo Waziri wa Mambo ya Nje na...
Viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwa katika picha ya pamoja na Mheshimiwa Rais katika Ufunguzi wa Mahakama hiyoWaziri wa Mambo ya Nje na Mbunge wa Jimbo la Mtama Mheshimiwa Bernad Kamilius Membe akihutubia wananchi wa Rondo-Mnara huku Rais wa Jamhuri ya Muungano, Mheshimiwa Jakaya Kikwete akimsikiliza katika Ufunguzi huo.Baadhi ya wananchi wa Rondo waliojitokeza kwa wingi katika Uzinduzi wa Mahakama ya Mwanzo ya Rondo- Mnara Wilaya ya Lindi vijijini, Mkoani Lindi.Wananchi mbalimbali waliojitokeza kumsikiliza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho kikwete katika Ufunguzi wa Zahanati ya Rondo, Mkoani Lindi.
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo amezindua Mahakama ya Mwanzo katika Eneo la Rondo Mnara Wilaya ya Lindi Vijijini Mkoani Lindi.
Mheshimiwa Rais ameambatana na Waziri wa mambo ya nje ambae pia ni Mbunge wa jimbo la Mtama mkoani humo Mheshimiwa Bernard K. Membe.
Katika Hotuba yake ya Ufunguzi Mheshimiwa Rais aliwataka wananchi wa Rondo kufuata utaratibu wa sheria katika kuwashughulikia waarifu wa makosa mbalimbali na kuchukua sheria mikononi. Mheshimiwa Rais pia alieleza katika hotuba yake hiyo kuwa mahakama ni muhimili mkubwa wa Serikali na hivyo ni vizuri ikitumika ipasavyo na kutoa haki kwa kila mtu.
Pia alimuita Diwani wa Eneo hilo na kumuuliza juu ya Changamoto na Kero za Eneo hilo na Diwani alitaja kuwa kero kubwa ni tatizo la Maji, barabara pamoja na kutokuwepo kwa Kituo cha Polisi, ambapo Mheshimiwa Rais alichangia shilingi milioni tatu 3,000,000.00 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha polisi na pia kumuagiza Mkurugenzi alete mabomba ya maji haraka katika Eneo hilo na pia akawahimiza makandarasi wa barabara kujitahidi kukamilisha Ujenzi huo haraka iwezekanavyo. 
Mheshimiwa Rais yupo katika ziara ya siku tano Mkoani Lindi ambapo leo joini atahutubia katika wilaya ya Ruangwa na Nachingwea.


About Author

Advertisement

 
Top