M23 wawasili Kampala kwa mazungumzo

Wapiganaji wa M23 wakiondoka GomaWaakilishi wa serikali ya Jamhuri ya Demokrasi ya Congo na wapiganaji wa M23 wanakusanyika mjini Kampala, Uganda, kwa mazungumzo.

Juma lilopita wapiganaji hao waliondoka kwenye mji wa Goma, lakini walitishia kuuteka tena iwapo madai yao hayatatimizwa.

Rais Joseph Kabila amesema atasikiliza malalamiko yao.

Watu zaidi ya nusu milioni wamekimbia makwao katika ghasia tangu wapiganaji hao walipoasi na kutoka katika jeshi la Congo mwezi wa Aprili.

Waziri wa taifa wa Uganda anayehusika na mashauri ya nchi za nje, Henry Okello Oryem, amesema kuwa mazungumzo hayo yanaweza kuendelea kwa miezi kadha kabla ya kufikia suluhu na maafikiano kutekelezwa.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post