Umoja wa Mataifa unasema kuwa jeshi la Sudan Kusini limewapiga risasi na kuwauwa watu 10, ambao walikuwa wakiandamana kupinga kuhamishwa kwa makao makuu ya serikali za mitaa magharibi mwa nchi.
Afisa wa kuweka amani wa Umoja wa Mataifa huko Bahr el-Ghazal amesema watu wane waliuwawa katika mji wa Wau kwenye mapambano ya jana usiku.
Na wengine sita waliuwawa baada ya kukusanyika kulalamika juu ya mauaji ya awali.
Jeshi la Sudan Kusini limekataa kusema kitu.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.