NIJUZE NIJUZE Author
Title: YANGA YAKUTANA TENA NA APR NUSU FAINALI-KAGAME CUP
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Mabingwa watetezi wa Kagame Cup Yanga leo ndani ya Uwanja wa Taifa Dar es Salaam walikabwa koo na Mafunzo ya Zanzibar kwenye Mechi ya Robo ...
Mabingwa watetezi wa Kagame Cup Yanga leo ndani ya Uwanja wa Taifa Dar es Salaam walikabwa koo na Mafunzo ya Zanzibar kwenye Mechi ya Robo Fainali na kwenda sare ya bao 1-1 katika Dakika 90 lakini wakaibuka kidedea kwenye tombola ya Penati Tano Tano waliposhinda Penati 5-3 na hivyo kutinga Nusu Fainali ambayo watacheza na APR ya Rwanda hapo Jumatano.
Mafunzo ndio waliotangulia kupata Bao katika Dakika ya 34 mfungaji akiwa Ally Othman Mmanga na Yanga kufanikiwa kusawazisha kwa bao la Said Bahanuzi la Dakika ya 46.
Lakini hadi Dakika 90 Mechi ikamalizika droo ya Bao 1-1 na ndipo ikaja Mikwaju ya Penati Tano Tano na Yanga wakafunga zote kupitia Said Bahanunzi, Nadir Cannavaro, Hamis Kiiza, Haruna Niyonzima na Athuman Idd.
Mafunzo walikosa Penati moja.
APR wamefanikiwa kuingia Nusu Fainali baada ya kuichapa URA ya Uganda bao 2-1 katika Mechi ya Robo Fainali ambayo ilitanguliwa kuchezwa hivi leo Uwanja wa Taifa kabla ya Mechi ya Yanga na Mafunzo.
Bao za APR zilifungwa na Iranzi na Ndikumana na la URA mfungaji ni Ssentongo.
Kwenye Nusu Fainali, Yanga na APR zitakuwa zikikutana kwa mara ya pili kwenye Mashindano haya baada ya kucheza Mechi ya Kundi C juzi Ijumaa na Yanga kuibamiza APR bao 2-0.

VIKOSI:
YANGA:
Yaw Berko, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub Cannavaro, Kelvin Yondani, Athuman Idd Chuji, Rashid Gumbo, Haruna Niyonzima, Said Bahanunzi, Hamis Kiiza, Stephano Mwasika
Akiba: Ally Mustapaha 'Barthez', Godfrey Taita, Ladislaus Mbogo, Juma Seif Kijiko, Idrisa Rashid, Shamte Ally, Jeryson Tegete
MAFUNZO:
Khalid Mahadhi Haji, Ismail Khamis Amour, Said Mussa Shaaban, Salum Said Shebe, Ali Othman Mmanga, Juma Othman Mmanga, Suleiman Kassim, Jaku Juma Jaku, Mohamed Abdulrahim, Wahid Ibrahim, Ally Juma Hassan
Akiba: Salum Mohamed Pangani, Haji Abdi Hassan, Kheir Salum Kheir, Sadik Habib Rajab, Thabit Mohamed Abdallah

RATIBA/MATOKEO:

ROBO FAINALI

Julai 23 Jumatatu

Mafunzo 1 Yanga 1 [Penati 3-5]

URA 1 APR 2

Julai 24 Jumanne

18 Atletico vs Vita Club

19 Azam vs Simba

NUSU FAINALI

Julai 25 Jumatano

20 Yanga vs APR

Julai 26 Alhamisi

21 Mshindi 18 vs Mshindi 19

Mshindi wa 3:

Julai 28 Jumamosi

Aliefungwa 20 vs Aliefungwa 21

FAINALI:

Julai 28 Jumamosi

23 Mshindi 20 vs Mshindi 21

About Author

Advertisement

 
Top