THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898 PRESIDENT’S OFFICE,
E-mail: ikulumawasiliano@yahoo.com THE STATE HOUSE
press@ikulu.go.tz P.O. BOX 9120
Fax: 255-22-2113425 DAR ES SALAAM.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, atawaapisha Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Kesho tarehe 13 April, 2012, saa 3 asubuhi katika viwanja vya Ikulu.
Tume itaanza kazi zake rasmi tarehe 1, Mei, 2012 kama ilivyopangwa na kutangazwa awali.
Kwa kuzingatia umuhimu wa shughuli hii, Nawaomba wahariri mtutumie majina ya waandishi waandamizi ambao watafika ikulu mapema saa 2.00 asubuhi kwa ajili ya shughuli hii.
Tunaomba majina hayo ya wawakilishi wa vyombo vyenu yawasilishwe kwetu mara baada ya kupata taarifa hii na mwisho wakupokea majina itakuwa saa 12.00 jioni ya leo .
Tunapenda kusisitiza kuwa waandishi watakaoruhusiwa kuhudhuria shughuli hii ni wale tu ambao tutapokea majina yao kutoka kwa wahariri wa vyombo husika.
Tunaomba ushirikiano wenu na karibuni.
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.