abdulaziz abdulaziz Author
Title: DKT Bilal Afungua chuo cha Veta Mkoani Lindi
Author: abdulaziz
Rating 5 of 5 Des:
Dk Mohamedi Gharib Bilal SERIKALI imevitaka vyuo vya ufundi stadi hapa nchi kutoa mafunzo kulingana ubora wa mafunzo kwa kuzingatia m...

DSC00157
Dk Mohamedi Gharib Bilal
SERIKALI imevitaka vyuo vya ufundi stadi hapa nchi kutoa mafunzo kulingana ubora wa mafunzo kwa kuzingatia mtazamo mpana na ushindani katika soko la ajira na mahitaji ya kimataifa katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia.
Wito huyo umetolewa na makamu wa rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dk Mohamedi Gharib Bilal wakati wa sherehe za uzinduzi wa chuo cha ufundi stadi (VETA) kilichojengwa eneo la eneo la Mitwero katika Manispaa ya Lindi.
Dk Bilal alisema kuwa serikali itaendelea kuweka msukumu katika kuhakikisha kwamba taifa linawekeza katika kutoa elimu na mafunzo ya ufundi stadi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wan je na ndani ili elimu na mafunzo ya ufundi yanawafikia vijana wengi kwa ajili ya ustawi wa jamii na taifa kwa ujumla.
Makamu wa rais huyo pia amezitaka mamlaka ya elimu na fundi stadi kuhakikisha inafanya tathimini ya kina kuhusu mahitaji ya kazi kwa kuzingatia kupanuka kwa uchumi katika sekta mbalimbali.
Aidha makamu wa rais aliwataka wananchi wa Mkoa wa Lindi kutumia kikamilifu fursa ya kuwepo kwa chuo hicho ambacho ni moja ya vyuo vichache vya kisasa hapa nchini, na kueleza kuwa tegemeo lake kubwa vijana wote wenye sifa husika kutoka wilaya zote za mkoa wa Lindi wanakujiunga na chuo hicho.
Nae Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya elimu na mafunzo ya ufundi stadi Muhandisi Zebadiah Moshi alisema ujenzi wa chuo hicho umegharimuni shs bilioni4.4 ambapo majengo shs bilioni 3 mitambo, vifaa vya mafunzo na samani shs bilioni 1.44 kati ya fedha hizo serikali ya Tanzania imetoa asmilia 60.9 na serikali ya korea asilia 39.1.veta
Mhandisi Moshi alisema kuwa chuo hicho kitakuwa na uwezo wa kutoa nafsi 400 za mafunzo ya muda mrefu na 800 za mafunzo ya muda mfupi kwa mwaka na kwamba chuo kina uwezo wa kuchuku wanafunzi wa bweni 120 kati yao 40 wasichana swa na aslimia 33.


JENGO

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top