Arsenal Chelsea nguvu sawa

ArsenalArsenal imegawana pointi na Chelsea katika mchezo wa Ligi Kuu ya England uliochezwa kwenye uwanja wa Emirates baada ya kutoka sare ya 0-0.

Chelsea wakiwa na mechi ngumu dhidi ya Barcelona siku ya Jumanne, walichezesha wachezaji kadhaa wa akiba ili kujaribu kujiandaa na mchezo wa Klabu Bingwa Ulaya.

Licha ya nafasi za hapa na pale kutoka pande zote mbili, mchezo huo ulikosa msisimko mkubwa kutokana na wachezaji kupoteza pasi na mipira kila mara.

Matokeo haya yanaiacha Arsenal katika nafasi ya tatu, ingawa matokeo ya Tottenham na Newcastle huenda yakaipa wasiwasi klabu hiyo ya kaskazini mwa London.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post