DC NANYUMBU ATANGAZA VITA NA WALANGUZI WA CHOROKO
Hatua hiyo ni katika jitihada ya serikali ya wilaya kuwasaidia wakulima zao hilo baada ya msimu uliopita kudhulumiwa na wafanyabiasha hao kwa nunua zao hilo kwa bei ya shs 300 kwa kilo moja na robo na kutumia vipimo visivyo rasmi maarufu (kangomba).
Agizo hilo alilitoa kwenye Mkutano wa watendaji, viongozi wa kimila (Mamwenye) na wananchi ulichofanyika tarafa ya Nakopi alipokuwa kwenye ziara ya kuhimiza na kuamasisha shughuli za maendeleo wilayani humo.Fatuma Ali alisema serikali imefanya jitihada za kukiamasisha chama kikuu cha ushirika wilayani humo (MAMKU) kununua zao kwa kutumia mfumo wa stakabadhi ghalani ili kuwasaidia walikuma wasiendelee kuibiwa na wajanja wa chache ambao wananunua kwa kutumia vipimo visivyo rasimi na bei dogo.
Alisema chama kikuu cha ushirika MAMKU kitakusanya choroko zote kwa wakulima kwa bei ya shs 800, baada ya kukusanya kitapeleka kwenye maghala makuu ambapo kutakuwa na mnada kwa wafanyabishara wanaohitaji kununua zao hilo.
Mkuu huyo wa wilaya ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama aliwaagiza watendaji vijiji na kata kuwajibika katika maeneo yao ili kuwathibiti kwa kuwakamata wanunuzi wote ambao wananunua kinyume na agizo hilo.
Fatuma aliwataka watendaji wote wilayani humo kufahamu kwamba sifa moja wapo ya mtuimishi wa umma kutojihusisha kwa namna yotote ya uvunjifu wa sheria na kusema kuwa kushirikiana na walanguzi kwa mtendaji ni kosa hivyo ni vyema watendaji wa vijiji , kata wakashirikiana na wananchi kuwafichua wanunuzi hao.
‘ndugu zangu na amini walanguzi wote tuna watambua kwani ni miongoni mwetu, kama sio ndugu zetu basi wajomba zetu hivyo ni vizuri sasa tukamua kwenda kuwashauri waache tabia hiyo ya kuwaibia ili kuweze kukomesha tatizo hili.’alisema mkuu huyo.
Mkuu huyo alisema ofisi yake haita kuwa tayari kuwavumilia watendaji wote watakaobainika kwa namna moja hama nyingine wana shirikiana na wanunuzi hao kwa kuwathulumu wananchi pia alitumia nafsi hiyo kuwa tangazia wananchi kuwa chama kikuu cha ushirika MAMKU kitaanza kununa zao kwa bei ya shs 800 muda wowote kuanzi sasa
Tags
kilimo