Unknown Unknown Author
Title: TATIZO LA KUKATIKA KATIKA KWA UMEME LINDI LATOLEWA UFAFANUZI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Umeme ni moja kati ya Nguzo kubwa katika kukuza Uchumi wa Nchi na kuongeza pato kwa mwananchi kwa kujishughulisha na mambo mbali mbali yan...
Umeme ni moja kati ya Nguzo kubwa katika kukuza Uchumi wa Nchi na kuongeza pato kwa mwananchi kwa kujishughulisha na mambo mbali mbali yanayoweza kumuingizia kipato kwa kutumia nishati hiyo.
tanesco
Katika kulitambua hilo Serikali imekuwa ikijitahidi kwa hali na mali kuhakikisha kuwa wananchi wake wanapata huduma bora ya Nishati hiyo kupitia Shirika la Umeme nchini Tanesco. Tumeshuhudia mambo kadha wa kadha katika kulifanya shirika hilo liweze kutoa huduma bora.

Lakini hali imekuwa Tofauti katika Mkoa wa Lindi kwa Takribani miezi kadhaa sasa wakazi wa mkoa huu wanapata adha ya Umeme ambayo inapelekea kuwaingiza katika hasara mbalimbali, kwa kukosa umeme wa uhakika.

Akizungumzia matatizo yaliyopo Afisa Habari wa Shirika la Tanesco Tawi la Lindi Mr. Francis Mbelwa amesema kuwa Kadhia hiyo inasababishwa na mambo kadha wa Kadha.

Moja ikiwa ni Uchakavu wa Miundo mbinu ya Usafirishaji wa Umeme, Pili Njia ya kusafirisia umeme kuwa Ndefu kutoka chanzo kikuu cha Kuzalishia Umeme (Mtwara) pamoja na kuwepo kwa michepuko mingi katika njia hiyo akitolea mfano Mikindani,  Madangwa,  Mpapura,  Kitunda,  Mnazi 1, Ng'apa,  na Kinengene.

Afisa habari huyo amebainisha kuwa michepuko mingi hiyo huleta changamoto hasa pale inapotokea hitilafu katima moja ya mchepuko kwani husababisha umeme kuzima katika njia yote. Hitilafu hiyo inaweza sababishwa kwa nyaya kuguswa na wanyama wadogo wadogo kwani njia hiyo ina msongo mdogo wa Kilo Volt 33.

Ndg: Mbelwa amebainisha kuwa Mashine kati ya Tisa ambazo zinatumika kuzalisha umeme Kiasi cha megawati 18 hivi sasa zimepungua uwezo kwani Mashine 2 hazifanyi kazi na zilizobaki zimepungua uwezo na kufanya kiasi cha Umeme kinachozaliswa kuwa Megawati 15 huku mahitaji yote kwa ujumla kuwa ni Megawati 14, hivyo wakati mwingine hupelekea kuzima kwa kuzidiwa uwezo.

Aidha Afisa huyo aliwataka wateja na wananchi wa mkoa wa Lindi kuwa na Ustahimilivu kwani Shirika la Umeme linafanya jitihada kumaliza tatizo hilo, hivi sasa wako mbioni kujenga njia mpya ya Umeme ya Msongo mkubwa wa Kilo Volt 132 ambayo kituo hicho kitajengwa katika kijiji cha Mahumbika.
power plant Mtwara
Mchakato wa Ujenzi huo hivi sasa umeshaanza kwa kujenga kituo Mtwara sehemu inayoanzia kuzalishwa umeme huo na amesema kuwa mnamo mwezi februari mwishoni njia yote itakuwa imekamilika na kuondoa adha ya Umeme katika Mkoa wa Lindi.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM
Usipitwe!! Ungana na Familia hii kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata Infortainment zote!! Usikose kujiunga na Youtube channel yetu ili kupata Exclusive mbalimbali kali kutoka LindiYetu TV

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top