Unknown Unknown Author
Title: SIMULIZI:: SITALIA TENA SEHEMU YA 21
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
SIMULIZI:: SITALIA TENA SEHEMU YA 21 MTUNZI: NYEMO CHILONGANI ILIPOISHIA.....!!!! “Saida...Saida...Saida mpenzi....” aliita Kareem huku a...
SIMULIZI:: SITALIA TENA
SEHEMU YA 21
MTUNZI: NYEMO CHILONGANI
SIMULIZI:: SITALIA TENA SEHEMU YA 21
ILIPOISHIA.....!!!!
“Saida...Saida...Saida mpenzi....” aliita Kareem huku akipekua huku na kule, kila alipopekua alikutana na mwili, katika miili yote hiyo aliyoiona, hakujua Saida alikuwa yupi kutokana na kuteketezwa na moto ule.

“Saida...Saida mpenzi usife...Saida...Saidaaa...” aliendelea kuita Kareem.


ENDELEA NAYO SASA....
Mauaji yalitanda kila kona, watu walikuwa wakijitoa mhanga kila siku, hakukuwa na amani, katika migahawa mingi ndani ya nchi za Ulaya na Marekani, watu waliogopa kukaa kwani kila siku kulikuwa na mauaji yaliyokuwa yakifanyika.

Dunia haikuwa na amani tena, kila kona kulikuwa na mauaji ya kujitoa mhanga, kila mmoja aliogopa kwani wengi walihisi kwamba mara baada ya Osama Bin Laden kuuawa, basi kusingekuwa na matukio ya kigaidi tena.

Magaidi wakajipanga, wakaamua kufanya mauaji kama kawaida, mauaji waliyosema kwamba ni visasi kwa kile walichokuwa wamefanyiwa na Wamarekani ambao kila siku walikuwa wakiwaonea, mbaya zaidi waliingia mpaka katika nchi zao na kuanza kuwatawala.

Iliwauma, mioyo yao ilichoma sana, kifo cha Osama hakikuwa mwisho wa mapambano, kama kawaida wakajipanga na watu kuendelea kujitoa mhanga kama kawaida kitu kilichoonyesha kwamba Osama aliacha virusi vya ugaidi vilivyoendelea kuenea kila siku katika mioyo ya Waarabu wengi.

Mtu ambaye kwa kipindi hicho alikuwa akisimamia kundi la kigaidi la Al Qaeda alikuwa Hamis Al Habsi, kijana mwenye sura nzuri, ya upole lakini alikuwa katili kuliko Waarabu wote waliobaki.

Mara kwa mara alikuwa akiwachukua vijana na kuwafundisha namna ya kutumia silaha, alikuwa na sehemu maalumu na vijana wake ambao kazi kubwa ilikuwa ni kuwalisha watoto maneno ya sumu ambayo iliwapelekea kuwachukia sana Wazungu na kuwaona kama mashetani wakubwa.

“Wanakuja na kuwaua wazazi wenu, wanawanyonga kikatili, kiongozi wetu aliyekuwa akilitumikia kundi hili kwa moyo mmoja, Osama, ameuawa kwa kudhalilishwa sana, ameuawa na kuzikwa baharini, hivi mmekwishawahi kuona mtu akizikwa baharini? Kwa Osama, mkombozi wetu alizikwa baharini,” alisema Hamis huku akionekana kuwa na uchungu mkubwa, akaendele:
“Pambana kwa ajili ya familia yako, pambana kwa ajili ya ndugu zako, tukiendelea kuwakaribisha watu hawa katika nchi zetu wataendelea kutuua kila siku. Wangapi wapo tayari kumuua Mzungu popote wanapomuona?” aliuliza Hamis na vijana wote kunyoosha bunduki zao za AK 47 juu kuonyesha kwamba walikubaliana naye kwa asilimia mia moja.

Katika kufanya upelelezi wake kupitia majasusi wa CIA, Marekani ikagundua kwamba mbali na Osama waliyefanikiwa kumuua pia kulikuwa na mtu mmoja ambaye alionekana kuwa hatari sana, huyu mtu alikuwa Hamis Al Habsi. 

Walitakiwa kupambana, walitakiwa kumpata na kumuua kwani kumuacha hai lilikuwa kosa kubwa ambalo lingeigharimu dunia kwani mtu huyo hakuwa rafiki, aliua kila kona, hakuchagua sehemu wala eneo.

Wakaingia kazini, haikuwa kazi nyepesi, walimtafuta sehemu zote kwa kutumia satalaiti zao, walitaka kukamata hata mawasiliano yao lakini walipopata taarifa kwamba hakuwa akitumia simu, wakahamia sehemu nyingine na kuanza kuifuatilia familia yao.

Walihangaika kwa miaka minne ndipo wakafanikiwa kumuona akiwa Saudi Arabia. Huko walikaribia kumuua lakini wakachemka na walipomfuatilia, wakagundua kwamba alikimbilia nchini Misri, ndani ya jumba moja la bilionea mkubwa, Bwana Faraq.

Hawakutaka kutuma jeshi kwenda kumkamata, walichokuwa wakitaka ni kulipua jengo zima usiku kwa kuamini kwamba angekuwa humo. Kitu cha kwanza ni kutuma kamera ndogo ambayo ilionekana kuwa kama nzi lakini ilipiga picha kali na kuzituma katika satalaiti ya Marekani na picha hizo kutumwa mpaka katika makao makuu ya CIA nchini Marekani.

Katika picha hizo waliweza kumuona kila mtu aliyekuwa ndani ya jumba hilo. Walimuona Mzee Faraq ambaye walijua kabisa kwamba alikuwa mfadhiri mkubwa wa vikundi vya magaidi na kitu kilichowapa furaha zaidi waliweza kumuona mpaka Hamis Al Habsi waliyekuwa wakimtafuta kila pembe ya dunia.

“We got him!” (tumempata) alisema mkuu wa CIA.
“Bomb him as soon as possible,” (mlipueni haraka iwezekanavyo).

Ilikuwa ni sauti kutoka upande wa pili, ilitoka ikulu ambapo walikuwa wakifautilia kila kitu kupitia katika televisheni yao kubwa iliyokuwa humo. Hakukuwa na muda wa kuchelewa, ikatumwa ndege ndogo (drone) ambayo ilikuwa ikikimbia zaidi ya kilometa elfu kumi kwa nusu saa kwenda nchini Misri.

Ilikimbia kwa kasi, ilipofika katika Bahari ya Mediterania, ikasimama juu kabisa na haikuwa kazi rahisi kuonekana. Mtu aliyekuwa Marekani ndiye aliyeiseti na kuipeleka alipotaka. 

Akaliweka bomu tayari kwa kulilipua jengo hilo. Hawakutaka kumuonea huruma mtu yeyote aliyekuwa ndani ya jumba hilo, yule aliyekuwa akiiongoza ndege hiyo, alichokifanya ni kubonyeza kitufe kimoja na bomu kutoka, lilikuwa likikimbia kwa umbali wa kilometa mia tano kwa saa.

“Three minutes to target,” (dakika tatu kumfikia mlengwa) ilisikika sauti ya mwanaume kwenye simu huku bomu likiendelea kuelekea Misri kutoka baharini.

Kila mtu alikuwa kimya, hakukuwa na mtu aliyekuwa akizungumza kitu chochote kile, walisimama huku wakiangalia jinsi bomu lile lilivyokuwa likiendelea kwenda kule lilipokuwa jumba lile.

“Two minutes to target,” (dakika mbili kumfikia mlengwa) ilisikika sauti ya mwanaume huyo kwa mara nyingine.
“One minute to target,” (dakika moja kumfikia mlengwa)
“Fifty seconds to target....thirty seconds to target...ten seconds to target....five seconds to target...two seconds to target....one second to target...” ilisikika sauti ya mwanaume huyo ambaye alikuwa akitaja sekunde zilizobaki kabla ya kulifikia jengo lile na kulilipua.

Baada ya kusema kwamba ilibaki sekunde moja, hapohapo bomu likalifikia jumba lile na kulilipua. Watu waliokuwa pembeni ya nyumba ile walibaki wakishangaa, ulikuwa mlipuko mkubwa ulioonyesha kwamba bomu lililolipua lilikuwa kubwa.

Picha za satalaiti kutoka katika eneo lile lilionyesha miili kadhaa ya watu wakiwa wamekufa baada ya kuungua vibaya, ilikuwa ngumu kuamini kama kulikuwa na mtu aliye hai kwani kila mmoja alikuwa chini na viungo vikiwa vimekatika.

“Target confirm...” (mlengwa amethibitishwa) alisema mwanaume mmoja baada ya kuipata picha ya mwili wa Hamis pale chini, japokuwa ulikuwa umeungua vibaya lakini kompyuta iliunganisha vinasaba na kugundua kwamba watu waliokuwa wameuawa, mmoja alikuwa Hamis, wote wakapiga makofi kwa shangwe kuonyesha walifurahia kwa kile kilichokuwa kimetokea.

***********************************
Saida alikuwa sebuleni amekaa wakati ameagana na Kareem ambaye alikwenda kumnunulia matunda. Pale alipokaa, hakuwa na amani kwani hakutakiwa kuonekana na Hamis ambaye angeuliza maswali kwamba huyo mwanamke alikuwa nani na alikuwa akifanya nini mahali hapo.

Alitaka kumuona mpenzi wake akirudi haraka iwezekanavyo na waelekee katika chumba cha chini kilichokuwa katika handaki. Alisubiri na kusubiri, alipanga kusubiri kwa dakika kumi lakini kitu cha ajabu alikaa kwa dakika ishirini, mwanaume huyo hakuwa ametokea mahali hapo kitu kilichomfanya kukata tamaa ya kuendelea kumsubiri mahali hapo.

Alichokifanya ni kusimama kwenye kochi na kuelekea chumbani. Alikuwa amechoka na aliamini kwamba kama Kareem angerudi mahali hapo, angemfuata chumbani humo.

Wakati akiwa amefika huko, ghafla akasikia mlio mkubwa, mchanga ukaanza kutitia chini na kuanza kukifunika chumba kile.

Hakujua ni kitu gani kilitokea, aliogopa mno, alijikuta akitetemeka tu ndani ya chumba kile. Wakati akijifikiria ni kitu gani alitakiwa kufanya ndani ya chumba kile, udongo ukaanza kuangukia katika handaki lile hali iliyoifanya sehemu nzima kujaa vumbi, na baada ya sekunde kama thelathini, handaki lote likafunikwa na udongo ule huku na yeye akiwa ndani, kifusi kikamfukia kwa juu, hakujua kitu gani kiliendelea baada ya hapo.

JE, nini kitaendelea?, Je, huo ndiyo mwisho wa Saida?
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
KUWA KARIBU NASI LINDIYETU.COM
Usipitwe!! Ungana na Familia hii kupitia FacebookTwitter na Instagram ili kupata Infortainment zote!! Usikose kujiunga na Youtube channel yetu ili kupata Exclusive mbalimbali kali kutoka LindiYetu TV

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top