RAYVANNY WA WCB AMPA SHAVU MSANII HUYU

Siku chache zilizopita hitmaker wa ngoma ya "Natafuta Kiki" Raymond (Rayvanny) kutoka WCB Wasafi alipata shavu la kufanyiwa interview katika kipindi cha Lavidavi cha Choice Fm.
Rayvanny na FobyKipindi ambacho kinaendeshwa na mmoja wa wanadada machachari katika mitindo hapa Bongo Gigy Money huku akiwa na mshkaji wake Mo-J.

Moja kati ya maswali ambayo aliulizwa Rayvanny ni pamoja na “Tofauti na ngoma zake, ni ngoma gani anaielewa sana na kuisikiliza mara kwa mara.”

Haikuwa rahisi kwa wengi kulitegemea jibu ambalo lilitoka mdomoni mwa Rayvanny, baada ya kujibu “Naipenda sana ngoma ya ‘Star’ yakwake Foby, naisikiliza mara kwa mara nikiwa nyumbani na hata kwenye gari yangu.”

Isingekuwa rahisi kwa Rayvanny kuzungumza hivyo endapo ngoma hiyo isingekuwa kali, kama hujafanikiwa kukipitishia macho kichupa cha ngoma hiyo unaweza kuplay hii video hapa chini.

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post