Na. Ahmad Mmow, Lindi.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) mkoa wa Lindi, Ali Mtopa amewalaumu maofisa ugani mkoani humu kuwa chanzo cha uzalishaji mdogo wa mazao ya kilimo na kilimo cha kuhahama.
Mtopa ambae pia anajulikana kwa jina la profesa wa siasa aliyasema hayo kwenye kikao cha kamati ya ushau mkoa(RCC) kilichofanyika mwanzoni mwa wiki hii katika manispaa ya Lindi. Mtopa alisema baadhi ya maofisa ugani hawawajibiki ipasavyo.
Hivyo kuwa ni chanzo cha uzalishaji mdogo wa mazao ya kilimo ingawa mkoa huu unaardhi kubwa nayenye rutuba. Alibainisha kwamba maofisa hao wangewajibika ipasavyo wakulima wangeweza kuzalisha kwa wingi katika maeneo madogo nawangeacha kilimo cha kuhamahama kinachosababisha uharibifu wa misitu.
Mtopa alisema ushahidi unaodhihirisha kuwa baadhi ya namaofisa hao hawawajibiki ni kitendo cha kutokuwa na mashamba yao wenyewe, ingawa wanaitwa mabwana na mabibi shamba.
"Anaitwa bwana shamba lakini hana shamba, sasa wananchi wanawezaje kuhamasika nakujifunza namna ya kulima kilimo cha kisasa. Tena hawawatembelei wakulima," alisema Mtopa.
Kutokana na hali hiyo alitoa wito kwa serikali kuwatambua na kuwachukulia hatua maofisa ugani wazembe ambao kwa makusudi wanakwamisha juhudi za serikali ya awamu ya tano yakutaka nchi ijitosheleze kwa chakula na kuokoa misitu isiharibiwe nakusababisha kugeuka jwangwa.
Mbali na maofisa ugani, mwenyekiti huyo alitoa wito kwa serikali kuitupia jicho miradi ya umwagiliaji iliyopo mkoani humu. Akibainisha kwamba baadhi ya miradi imetumia fedha nyingi lakini haijaisha na hakuna matarajio kama miradi hiyo itakamilika kama ilivyotarajiwa.
"Kama ule mradi wa Ngongowele kule Liwale ni kaburi la fedha za serikali, zimetumika fedha nyingi lakini hakuna kilichofanyika. Afadhali mradi wa Mtawango ukiuona unaridhika kabisa lakini sio ule wa Ngongowele na ipo mingi ya aina ile," alisema Mtopa.
Aliongeza kusema hali hiyo isipodhibitiwa itakuwa ni vigumu kufanikiwa dhamira njema ya serikali. Hivyo serikali inakila sababu ya kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa miradi hiyo ili ijiridhishe kama matumizi ya fedha yanalingana na kazi zilizofanyika. Badala ya kuendelea kutia fedha zinazotokana na kodi za wananchi bila kufuatilia na kujiridhisha.
Kwa upande wake, mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi alikiri kuwa baadhi ya watumishi hawawajibiki ipasavyo. Ambapo wengine wanaishi nje ya vituo vyao vya kazi.
Alisema hali hiyo haikubaliki na haiwezi kuvumiliwa. Nakutahadharisha kwamba wanatakiwa wabadilike haraka kwani kila mtumishi anatakiwa aende na kasi ya utendaji wa serikali ya awamu ya tano.
********
Post a Comment Blogger Facebook
Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii
Note: Only a member of this blog may post a comment.