MKURUGENZI WA JAMII FORUMS HATIMAE ASOMEWA MASHITAKA NA KURUDISHWA RUMANDE

Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, kampuni inayomiliki mtandao maarufu, Jamii Forums, Maxence Melo ameshtakiwa kwa Makosa 3 likiwemo la kuendesha na kumiliki tovuti ambayo haijasajiliwa hapa nchini kinyume cha sheria.
Maxence Melo
Shitaka lingine ni kuzuia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi chini ya kifungu cha 22 cha Sheria ya Makosa ya Kimtandao pamoja na kusajili tovuti ya Jamii Forums kwa kikoa cha .com badala ya .co.tz jambo ambalo serikali inadai ni kinyume cha sheria.

Kati ya mashitaka hayo matatu, mashtaka mawili amepata dhamana na lakini katika shtaka la 3 amekosa dhamana ambapo kabla hajakamilishiwa dhamana ya shtaka la tatu Melo ameondolewa mahakamani na kupelekwa gereza la Keko.

Taarifa kutoka mahakamani hapo zinadai kuwa wadhamini wa shtaka la tatu walikuwa wamepatikana ndani ya muda lakini upande wa Jamhuri ulikua umeshaondoka.


**********

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post