SHILOLE AJIGAMBA KUMFUNIKA YEMI ALADE KATIKA JUKWAA LA FIESTA 2016 IMOOOOOOO....!!!!!

Kuelekea November 5 kwenye kilele cha ule msimu wa Burudani Tanzania Fiesta 2016, mwanadada Shilole amejigamba kumfunika msanii wa kimataifa kutoka nchini Nigeria Yemi Alade kwa performance kali usiku huo.
Shilole na Yemi Alade
Msanii huyo ameyasema hayo leo hii pande za THT wakati wasanii ambao wanatarajia kuperform kwa Live Band walipokuwa wakifanya mazoezi ili kuhakikisha wanapiga show kali usiku huo.

Shilole alikuwa mmoja kati ya wasanii hao, ndipo informer wa Lindiyetu.com akaona itakuwa poa kama akipiga nae story na kujua amejipanga vipi katika kutoa burudani usiku wa November 5 pande za Leaders Club.

“Mazoezi yako poa, nimejipanga kuingia na dancers zaidi ya 10 kwenye stage siku hiyo, nimeandaa surprises kibao kwa mashabiki wangu. Kama msanii lazima niwe na surprises za kutosha, kuna vitu vingi sana verry amazing. Miaka 3 iliyopita alikuja Yemi Alade lakini alinikimbia, sasa round hii kaja tena katika staje ya Fiesta namnyoosha.” alijigamba Shilole.
************ 

Post a Comment

Hii ni Blog kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Nchi yetu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...

Previous Post Next Post