Unknown Unknown Author
Title: LIWOPAC LAUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI KUOKOA MAISHA YA WATOTO WACHANGA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na. Ahmad Mmow, Lindi. Katika kuhakikisha vifo vya watoto wachanga vinatokomezwa, shirika la kutoa msaada wa kisheria kwa wanaweke na wa...
Na. Ahmad Mmow, Lindi.
Katika kuhakikisha vifo vya watoto wachanga vinatokomezwa, shirika la kutoa msaada wa kisheria kwa wanaweke na watoto la Lindi (LIWOPAC) limepanga kuunga mkono juhudi za serikali za kutokomeza vifo vya watoto mkoani humu.
LIWOPAC - Lindi
Hayo yalielezwa na ofisa mwandamizi wa shirika hilo, Pius Phinias kwenye mdahalo wa utekelezaji wa mradi unaoitwa OKOA MAISHA YA MTOTO MCHANGA KWA MAENDELEO ENDELEVU LINDI. Yaliyofanyika hivi karibuni katika manispaa ya Lindi.

Pius ambae shirika lake la LIWOPAC lilianza kufanyakazi mwaka 2001, alisema limeamua kuunga mkono juhudi za serikali za kuokoa maisha ya watoto kwa kuanzisha mradi huo ili kutokomeza vifo vya watoto wachanga vinavyoweza kuepukika.

Pius ambae pia ni ofisa wa mradi huo, alibainisha kwamba mradi huo utajikita kulinda haki za binadamu ya kuishi. Kwasababu watoto wachanga wanafanyiwa vitendo vya kikatili na wazazi wao kwa kukusudia au bahati mbaya.

Hivyo kuwasababishia ulemavu au kupoteza maisha.
"Mkoa wetu wa Lindi nimiongoni mwa mikoa yenye changamoto kubwa ya vifo vya watoto wachanga, ambapo watoto 60 hadi 80 kati ya watoto 1000 hufariki dunia kila mwaka ndani ya siku saba tangu kuzaliwa," alisema Pius.

Aliyataja maeneo ambayo yataanza kunufaika na mradi huo ambao utekelezaji wake utafanyika kwa kipindi cha miezi sita ni wilaya za Kilwa na Lindi. Ambapo katika wilaya ya Lindi, kata za Nangaru, Milola na Nyangamara zitafikiwa na kunufaika na mradi huo.

"Mradi huu utaanza kutekelezwa mwaka huu na kumalizika mwakani, kipindi hicho nichamatazamio, Mradi huu unaofadhiliwa na mfuko wa msaada wa kisheria (FCS) utagharimu shilingi 72.00 milioni zitakazotolewa kwa awamu mbili," alibainisha Pius.
LIWOPAC - Lindi
Alisema malengo ya mradi huo ni kuhakikisha wananchi wanaoishi katika wilaya hizo waweze kuzijua changamoto zinazosababisha vifo vya watoto wachanga, kupunguza idadi ya vifo vinavyoepukika, uwepo wa mabalozi wa kujitolea watakaoweza kutoa huduma ya ushauri na dharura kwa akinamama wajawazito na kuongeza uwajibikaji wa viongozi wa serikali za mitaa katika kusimamia utoaji wa huduma bora za afya.

Kwa upande wake, mkurugenzi wa shirika hilo, Cosma Bulu alisema kumekuwa na dhuluma kubwa za haki za wanawake na watoto, hasa za msingi. Ikiwamo unyanyasaji wa kijinsia, uonevu na ukatili ambao mara nyingi unafanywa na wanaume dhidi ya wanawake.

Hivyo jamii inatakiwa kuwa mstari wa mbele katika kusaidia kutatua changamoto hizo zinazowakabili.
"LIWOPAC inaendelea kupokea malalamiko kutoka kwa watu mbalimbali ambao wanaamini haki haitendiki au wenyewe hawajatendewa haki," alisema Bulu.

Kwa upande wao baadhi ya washiriki kwenye mafunzo hayo walishauri serikali itoe elimu ya uzazi shuleni. 

Ambapo wengine walitoa wito serikali za vijiji zitunge sheria zitakazo tumika kuwadhibiti wanaochangia vifo vya watoto na akina mama wajawazito.

Hamisi Maluka kutoka kata ya Nangaru, alisema elimu ya uzazi na umuhimu wa akina mama wajazito kuhudhuria kliniki ianze kutolewa shuleni badala ya kwenye maeneo ya kutolea huduma za afya pekee. 

Alisema elimu hiyo ikitolewa shuleni itawajengea uelewa wanafunzi kuhusu uzazi wa mpango na sababu zinazosababisha vifo vya watoto na wajawazito na njia sahihi za kuepusha vifo hivyo.
"Watunga sera hawanabudi kuhakikisha elimu hiyo inafikishwa na kufundishwa shuleni,kwakufanya hivyo tutaokoa maisha hata ya vizazi vijavyo," alisema Hamisi.
LIWOPAC - Lindi
Ofisa mtendaji wa kijiji cha Nangaru, Yousuf Masoud alishauri vijiji vitengeneze sheria zitakazotumika kuwadhibiti wanaodumisha mila potofu zinazosababisha vifo vya watoto na akinamama wajawazito.

Alisema zisipotungwa sheria hakutakuwa na ufanisi utakaotoa matokeo mazuri ya juhudi zinazofanyika. Kwamadai kwamba baadhi ya wananchi ni wakaidi.

Muuguzi wa zahanati ya Nyangamara, Tusajigwe Mbunda, alisema wanaume nikikwazo katika kusambaza elimu kuhusu uzazi wa mpango na masuala mengine yanayohusu afya za akinamama wajawazito na watoto wachanga. Kwamadai kuwa wasikilizaji wanaosikiliza na kupata elimu ni wanawake tu. Kwasababu wanaume hawataki kwenda kliniki hata wakezao wanapokuwa wajawazito.

Hivyo alishauri juhudi kubwa za kuwafikishia elimu mahali walipo zifanyike ili waweze kubadili mtazamo.

Mafunzo hayo ya sikumoja yaliwashirikisha baadhi ya wataalamu wa afya, viongozi wa kisiasa na dini, watendaji wa vijiji na kata, vijana na wazee kutoka katika kata za Nangaru, Milola na Nyangamara. Ambazo zipo katika wilaya ya Lindi.
**********

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top