NIJUZE NIJUZE Author
Title: RPC - CUP LINDI: RAHALEO YAIGARAZA MTANDA A, MASHINDANO YAFUNGULIWA RASMI NA KAMANDA RENATA MZINGA
Author: NIJUZE
Rating 5 of 5 Des:
Mshindano ya RPC Manispaa ya Lindi yameendelea leo kwa Kuzikutanisha Timu za Kata ya Mtanda A na Rahaleo, katika Mchezo huo Rahaleo waliibu...
Mshindano ya RPC Manispaa ya Lindi yameendelea leo kwa Kuzikutanisha Timu za Kata ya Mtanda A na Rahaleo, katika Mchezo huo Rahaleo waliibuka na Ushindi wa jumla ya Magoli 3-2.
Mtanda A Vs Rahaleo
Mpambano huo ambao ulichezwa majira ya saa 4:30jioni yaliweza kuhudhuriwa na Kamanda wa Polisi Renata Mzinga ambaye alikuwa kama Mgeni rasmi wa Mashindano hayo na aliweza kuyafungua rasmi, Mkuu wa wilaya ya Lindi pia alihudhuria Ufunguzi huo wa Mashindano.

Mechi ilikuwa na Upinzani makali na Timu zote ziliweza kuonesha kandanda safi lakini ilikuwa ni siku ya wakazi wa kata ya Rahaleo kutoka kifuambele dhidi ya wale wa Mtanda A.
Mtanda A Vs Rahaleo
Magoli ya Mtanda yalifungwa Mnamo dakika ya 25 na 40 ya kipindi cha Kwanza kupitia kwa wachezaji wake Ally Mbande pamoja na Goli la Kujifunga kupitia kwa beki Sadat Milinje.

Magoli ya Rahaleo yaliwekwa kimiani na Jamal Hassani mnamo dakika ya 6 Michael Mlekwa dakika ya 48 na Goli la Ushindi lilipatikana kupitia kwa Abuu Kipara mnamo dakika ya 75 ambaye aliibuka pia shujaa wa Mchezo huo na kuzawadia Simu ya Mkononi na Kampuni ya Halotel.

Mtanda A Vs Rahaleo
Abuu Kipara akipokea zawadi yake ya Simu ya Mkononi kutoka kwa Kampuniya simu ya Halotel aliyozawadiwa kama Mchezaji bora wa mechi hiyo.
Mtanda A Vs Rahaleo
Kikosi cha Kwanza cha Timu ya Rahaleo kilichocheza dhidi ya Mtanda A leo hii uwanja wa Ilulu katika Mashindano ya RPC Lindi.
Mtanda A Vs Rahaleo
Kikosi cha Kwanza cha Timu ya Mtanda A kilichocheza dhidi ya Rahaleo leo hii uwanja wa Ilulu katika Mashindano ya RPC Lindi.

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top