NINI TAFSIRI YA SHILOLE KUFUTA TATTOO YA MPENZI WAKE NUH MZIWANDA KIFUANI KWAKE, JE NIKWELI WAMEMWAGANA?

Kuna taarifa mtaani kuwa Penzi la Mastaa wa muziki, Shilole na Nuh Mziwanda limevunjika. Japokuwa sio mara ya kwanza kwa tetesi kama hizo kuhusu couple hiyo, lakini safari hii kuna dalili kuwa inaweza kuwa ‘serious’.
Shilole
Moja ya vitu vinavyoongeza nguvu ya tetesi hizo, Shishi amefuta ile tattoo aliyochora kifuani kwake miezi kadhaa iliyopita, yenye jina la ‘Nuh’ na kuchora UA juu yake.

Kipindi cha karibuni wawili hao hawaonekani pamoja kama ilivyozoeleka, na kila mmoja amefuta picha zao za pamoja kwenye akaunti zao za Instagram.

Shilole 
Pia weekend iliyopita Shishi alifanya sherehe nyumbani kwake ambayo hakusema sababu ya sherehe hiyo, lakini hakuwa na Nuh na wala hakupenda kumzungumzia pale alipoulizwa na marafiki aliowaalika.
Previous Post Next Post