HALI NI TETE: WAFUASI WA CCM na CHADEMA WACHOMANA VISU TUNDUMA

Vurugu Tunduma
Watu wawili wamefariki dunia baada ya vurugu kubwa kutokea kati ya wafuasi wa CCM na CHADEMA katika mji mdogo wa Tunduma Mkoani Mbeya.

Vurugu hizo zimetokea baada ya wanachama wa CCM kuweka mawe barabarani ili wafuasi wa CHADEMA wasipite kuhudhuria mkutano wa Lowassa.

Hali hiyo iliwafanya wafuasi wa CHADEMA kushuka ili kutoa mawe hayo, ndipo akatokea kijana mmoja wa CCM na kumchoma kisu kijana mmoja wa CHADEMA ambaye alifariki dunia papo hapo.
Vurugu Tunduma

Baada ya tukio hilo, vijana wa CHADEMA nao walijibu mapigo kwa kumshambulia na kumuua kijana huyo.

CHANZO:: PAPARAZI BLOG
Previous Post Next Post