Unknown Unknown Author
Title: BARAZA KUU LA WAISLAMU MKOA WA MWANZA LAMUONYA ASKOFU GWAJIMA.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Jana Ijumaa ya Octoba 16,2015 Baraza Kuu la Waislamu Mkoa wa Mwanza liliungana na Waislamu wengine kuadhimisha mwaka mpya wa Kiislamu amb...
Sherehe ya Mwaka mpya wa Kiislamu (1437)
Jana Ijumaa ya Octoba 16,2015 Baraza Kuu la Waislamu Mkoa wa Mwanza liliungana na Waislamu wengine kuadhimisha mwaka mpya wa Kiislamu ambao ni 1437. 

Kwa kalenda ya Kiislamu sherehe hizo zilifanyika jana tarehe mbili, mwezi Muharamu mwaka wa 1437 (02.01.1437) ikiwa maadhimisho yanayoambatana na kumbukumbu ya Kuhama kwa Mtume Muhammad kutoka Mji wa Macca kwenda Madina.

Na:George Binagi-GB Pazzo
Katika kuadhimisha sherehe hizo, Baraza hilo kupitia kwa Katibu wake Mkoani Mwanza Sheikh Mohamed Balla (Kulia Pichani) alitoa tamko kwa niaba ya Waislamu wote Mkoani Mwanza kutokana na kauli inayoelezwa kutolewa na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima kwamba ana ndoto ya Misikiti yote nchini kugezwa kuwa Sunday School na Masheikh watakwenda kuangukia katika misalaba.

Alisema kauli za namna hiyo si njema kwa mstakabali wa Taifa ambapo alisema kuwa Waislamu wote Mkoani Mwanza wanalaani na kukemea kauli hiyo na nyingine zote za aina hiyo na wale wanaozitoa.

Aliwataka Watanzania kuungana kwa pamoja hususani katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu na kwamba Wamchague kiongozi muadilifu, Mchapakazi na anaechukia rushwa ambae ataendelea kuwaunganisha watanania wote.

Sherehe ya Mwaka mpya wa Kiislamu (1437)
Imam wa Msikiti Khadija Jijini Mwanza Mohammed Awadhi akisoma Ibada ya Quran katika Sherehe za Mwaka mpya wa Kiislamu ulioadhimishwa jana katika Uwanja wa Mbugani Jijini Mwanza na kuambatana na ibada mbalimbali ikiwemo kuliombea taifa amani.Sherehe ya Mwaka mpya wa Kiislamu (1437)
Sheikh Mahamood Khasan akisoma ibada ya kuliombea taifa amani katika Sherehe za Mwaka mpya wa Kiislamu ulioadhimishwa jana katika Uwanja wa Mbugani Jijini Mwanza na kuambatana na ibada mbalimbali ikiwemo kuliombea taifa amani.
Sherehe ya Mwaka mpya wa Kiislamu (1437)
Imam wa Msikiti wa Ibadhi Jijini Mwanza Nouh Othman akisoma mada juu ya mwaka mpya wa kiislamu wa 1437 katika Sherehe zilizofanyika jana katika Uwanja wa Mbugani Jijini Mwanza na kuambatana na ibada mbalimbali ikiwemo kuliombea taifa amani.Sherehe ya Mwaka mpya wa Kiislamu (1437)
Qaswida
Sherehe ya Mwaka mpya wa Kiislamu (1437)
Qaswida
Sherehe ya Mwaka mpya wa Kiislamu (1437)
Waumini wa dini ya kiislamu wakiwa katika Sherehe za Mwaka mpya wa Kiislamu ulioadhimishwa jana katika Uwanja wa Mbugani Jijini Mwanza na kuambatana na ibada mbalimbali ikiwemo kuliombea taifa amani.
Sherehe ya Mwaka mpya wa Kiislamu (1437)
Waumini wa dini ya kiislamu wakiwa katika Sherehe za Mwaka mpya wa Kiislamu ulioadhimishwa jana katika Uwanja wa Mbugani Jijini Mwanza na kuambatana na ibada mbalimbali ikiwemo kuliombea taifa amani.
Sherehe ya Mwaka mpya wa Kiislamu (1437)
Waumini wa dini ya kiislamu Mkoani Mwanza wakiwa katika Sherehe za Mwaka mpya wa Kiislamu (1437) ulioadhimishwa jana katika Uwanja wa Mbugani Jijini Mwanza na kuambatana na ibada mbalimbali ikiwemo kuliombea taifa amani.
Sherehe ya Mwaka mpya wa Kiislamu (1437)
Waumini wa dini ya kiislamu Mkoani Mwanza wakiwa katika ibada ya Sherehe ya Mwaka mpya wa Kiislamu (1437) ulioadhimishwa jana katika Uwanja wa Mbugani Jijini Mwanza na kuambatana na ibada mbalimbali ikiwemo kuliombea taifa amani.

About Author

Advertisement

 
Top