Unknown Unknown Author
Title: NCCR-MAGEUZI KWAFUKUTA CHINI KWA CHINI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa NCCR-MAGEUZI, Mohammed Tibanyendela akizungumza na waandishi wa habari masuala mbalimbali ikwemo vi...
NCCR-MAGEUZI
Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa NCCR-MAGEUZI, Mohammed Tibanyendela akizungumza na waandishi wa habari masuala mbalimbali ikwemo viongozi wa juu kufanya kikao kinyemela leo Makao Makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mjumbe wa Baraza la Wadhamini,Thomas Nguma.
NCCR-MAGEUZI
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa NCCR-MAGEUZI,Mohammed Tibanyendela katika ofis za Makao Makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam.

Na.Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
CHAMA cha NCCR-MAGEUZI kimesema mkutano uliofanyika jana katika hoteli ya Land Mark jijini Dar es Salaam na Makamu Mwenyekiti pamoja na Katibu Mkuu wa chama hicho hawajajua lengo lake kutokana na kutokwepo kwa baraka ya vikao kwa mujibu wa chama hicho.

Akizungumza leo na waandishi habari jana Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa Chama hicho, Mohamed Tibanyendela amesema kuwa mkutano huo hujafanyika kwa kufuata taratibu hivyo wanaamini kuwa walikuwa wanazungumza masuala yao wenyewe na sio masuala yanayohusiana na chama hicho.

Amesema kuwa Makamu Mwenyekiti na Katibu ndio watendaji katika uendeshaji wa vikao vya chama lakini hadi wanakwenda kuzungumza na waandishi wa habari hakuna taarifa ya maandishi katika ofisi hiyo.

Tibanyendela amesema kama kumekuwepo na manung'uniko katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) suala hilo lingezungumzwa ndani ya vikao kutokana na viongozi waliozungumza walikuwa wakishiriki katika vikao vya UKAWA.

Amesema kuwa kikao kinachotambulika kilifanyika Septemba 16 katika ofisi ya chama lakini kufuatia na kikao cha jana hakikuwepo hivyo watakwenda tafsri katiba juu ya viongozi kuzungumza masuala ya chama bila kuwepo kwa vikao vinavyotambuliwa kikatiba.

Aidha amesema kuwa katika harakati zozote lazima kutakuwa na milima na tambalale yote haya ni kwa ajili ya kuitoa CCM madarakani.

Kamishina wa Tanga wa Chama hicho ,Ramadhan Mnyeko ambaye alikuwa katika kikao hicho amesema kuwa yeye aliitwa na Mwenyekiti lakini alikuwa hajui anaitiwa nini katika hoteli ya Land Mark.

Amesema gharama za kuja Dar es Salaam amejilipia mwenyewe kwani na taarifa ya kufika alipigiwa simu na sio barua.
source: Michuzi Blog

About Author

Advertisement

 
Top