Unknown Unknown Author
Title: CANNAVARO ASEMA HANA HOFU NA MSENEGAL WA SIMBA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mshambuliaji Msenegal, Pape N’daw. Wilbert Molandi, Dar es Salaam SIKU chache baada ya Simba kutangaza kumsajili mshambuliaji Msenegal,...
Pape N’daw
Mshambuliaji Msenegal, Pape N’daw.
Wilbert Molandi, Dar es Salaam
SIKU chache baada ya Simba kutangaza kumsajili mshambuliaji Msenegal, Pape N’daw, safu ya ulinzi ya Yanga inayoongozwa na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Kelvin Yondani, imeweka mipango kabambe ya kuhakikisha mchezaji huyo hafurukuti siku wakikutana.

Pape ambaye ana urefu unaokadiriwa kuwa futi 6.6, alisajiliwa siku kadhaa zilizopita kwa dau la dola 10,000 (Sh milioni 20).

Cannavaro ambaye ni nahodha wa Yanga, amesema kuwa safu yao ya ulinzi inazidi kuwa imara kutokana na kucheza pamoja kwa muda mrefu, hivyo hawana hofu juu ya mchezaji yeyote katika ligi.
“Hatumjui huyo mchezaji (Pape) lakini sisi tupo tayari kwa lolote na siyo kuwa tupo tayari kwa mchezaji wa ligi kuu tu, hata wa nje tupo tayari,” alisema Cannavaro.

Aliongeza kuwa kama aliweza kupambana na washambuliaji wenye majina makubwa kama Mamadou Niang, Demba Ba, El Hadji Diouf na Henry Camara kwenye Kombe la Mataifa Afrika (Afcon) mwaka 2008, ndiyo amshindwe Pape! Hilo ni gumu kwake.
“Wapo wengi tu wakali tumepambana nao, mfano kina Didier Drogba na wengine kibao, hivyo hatuna hofu. Soka limebadilika, zamani ukisikia mchezaji anatoka Senegal, Cameroon na Ghana unakuwa na hofu".
“Wengine wanaokuja ni wa kawaida tu, wanachukua fedha nyingi na bado hawaonyeshi kiwango cha maana. “Kikubwa ninachokwambia ni kwamba safu yetu ya ulinzi ipo vizuri. Imecheza pamoja kwa muda mrefu kwa kuanzia timu ya taifa na Yanga, ikiongozwa na mimi pamoja na Yondani".
“Kama nahodha wa Yanga na timu ya taifa kila wakati ninakaa pamoja na Yondani na kuwepo mipango thabiti kuhakikisha timu yetu hairuhusu mabao golini kwetu tukiwa kwenye klabu yetu na Stars,” alisema Cannavaro.

About Author

Advertisement

 
Top