Profesa Ibrahimu Lipumba akizungumza jambo katika moja ya Mikutano yake ya hadhara kwa wananchi.
ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi, CUF Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba amejiuzulu nafasi yake ya uwenyekiti. Prof. Lipumba amejivua nafasi hiyo leo asubuhi jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Picock ya jijini Dar es Salaam. Katika moja ya sababu alizoeleza zimemfanya ajiuzulu ni kitendo cha UKAWA kumsimamisha Edward Lowassa kama mgombea urais kupitia CHADEMA jambo ambalo yeye analipinga.
Alisema lengo la UKAWA ilikuwa kupinga katiba pendekezi ambayo imepitishwa na CCM akiwemo Lowassa ambaye hata kama atafanikiwa kushinda urais awezi kubadili katiba pendekezwa kwakuwa aliiunga mkono kuipitisha. Hata hivyo hali ya kujiuzulu ya kiongozi huyo ilijionesha tangu jana kwenye Ofisi za Chama hicho jijini Dar es Salaam ambapo alitaka kuzungumza na wanahabari lakini alizuiliwa na baadhi ya wanachama.
Taarifa zaidi juu ya habari za kujiuzulu kiongozi huyu ni hapo baadaye.