Na.Ahmad Mmow, Nachingwea.
Jinamizi la kuangushwa katika chaguzi limeendelea kumuandama waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mathias Chikawe, kubwagwa kwenye kura za maoni za ubunge wa jimbo la Nachingwea kupitia Chama Cha Mapinduzi.
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mathias Chikawe
Chikawe ambaye mwaka 2012 aliangushwa ndani ya chama hicho alipogombea ujumbe wa halmashauri kuu ya taifa kutoka wilaya ya Nachingwea. Mara hii ameangushwa tena katika kinyang'anyiro cha kura za maoni baada ya kuwa omba ridhaa wanachama hicho ili awe mgombea kwa awamu ya tatu.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo. katibu wa CCM wa wilaya ya Nachingwea, Leticia Mtimba, alimtangaza Hassan Elias Masala(36) mkuu wa wilaya Kibondo kuwa mshindi baada ya kujinyakulia kura 6494, aliyefuatiwa na Chikawe aliyepata kura 5128,.
Akiwashukuru wananchi na wanachama waliokwenda katika ofisi hiyo kusikiliza tangazo hilo ambao walilazimika kusubiri matokeo hayo toka saa tatu asubuhi hadi saa 11 jioni. Alisema anayodhamira ya kweli ya kweli yakuwahudumia wananchi kama alivyohaidi wakati anajinadi wakati wakampeni.
"Nikibahatika kushinda kwenye uchaguzi mkuu, sitambagua yeyote bali nitatekeza yale niliyohaidi na ambayo yalinisukuma kuomba ridhaa yenu wanachama wenzangu" nitashirikiana na kupata ushauri kutoka kwenu wanachama wenzangu,wananchi,viongozi wenzangu na walionitanguli katika nafasi ya ubunge iwapo nitachaguliwa katika uchaguzi ujao," alisema Masala.
Wagombea wengine na idadi ya kura za kwenye mabano ni Issa Mkalinga(469), Amandus Chinguile (1274), Issa Mkalinga(469) Ally Nanjundu(319) Fadhil Liwaka(1171) Albert Mnali(763) Beno Ng'ittu(797) Mustafa Maliche(427) Steven Nyoni (1438) Gaston Fransis 671.
Hii ni mara ya pili kwa waziri Chikawe kushindwa uchaguzi, kwani 2012 aliangushwa katika uchaguzi alipojaribu kutetea nafasi ya ujumbe wa halmashauri kuu ya taifa wa Chama Cha Mapinduzi mwaka 2012 baada ya kuangushwa na Fadhili Liwaka(32)