Unknown Unknown Author
Title: SIMBA SC YAINYUKA ZANZIBAR KOMBAIN 2-1, UWANJA WA AMAN ZANZIBAR
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Timu ya wekundu wa msimbazi, Simba Sc chini ya kocha mwingereza dlyan kerr, leo imeumana vikali na kombaini ya Zanzibar Mchezo ulipigwa kat...
Timu ya wekundu wa msimbazi, Simba Sc chini ya kocha mwingereza dlyan kerr, leo imeumana vikali na kombaini ya Zanzibar Mchezo ulipigwa katika uwanja wa amaan mjini zanzibar, mchezo huo ni sehemu ya maandalizi ya timu ya Simba katika mechi yake dhidi ya Afc Leopalds ya Kenya kwenye tamasha la kuwatambulisha wachezaji wake wapya waliowasajili katika msimu wa 2015/2016.
Simba day
Tamasha hilo ni maarufu kama Simba day, mchezo huo utapigwa kwenye dimba la taifa la dar es salaam tarehe 8 agosti 2015. Timu ya Simba inatarajia kuwatambulisha rasmi wachezaji wake wapya kama akina Hamisi Kiiza maarufu kama "diego", Mussa Hassani Mgosi, Mavugo, na wengineo.

Kocha Kerr ameutumia mchezo huu kama kipimo cha kutambua ubora wa kikosi chake kabla ya mechi hiyo ya Simba Day na AFC Leopalds na ligi ya VPL inayotarajia kuanza mwezi septemba.

Katika mchezo huo ambao ulikuwa wakushambulia kwazamu kila timu ilikuwa inatafuta udhaifu watimu pinzani ilikupata magoli ya mapema lakini hata hivyo simba iliwezakufanikiwa kuifunga Zanzibar Kombaini goli 2-1 na magoli hayo yalifungwa na wakongwe Mussa Hassani Mgosi na Hamisi Kiiza "Diego". Goli pekee la Zanzibar Kombaini limefungwa na Makame Mwinyi.

Kwa mchezo huo kocha wa Simba Sc ameweza kuona makosa yaliyopo katika Kikosi chake na ameiambia Lindiyetu.com kuwa makosa hayo yatarekebishwa kabla ya mechi yao ya Simba Day na AFC Leopard na kabla ya kuanza kwa mashindano ya ligi ya Vodacom Tanzania.

About Author

Advertisement

 
Top