VYAMA vya Siasa nchini katika kuelekea Uchaguzi Mkuu vimetakiwa katika ilani zao, kuweka vipengele vya watoto kutokana na kuwepo kwa sheria kandamizi dhidi ya mtoto.
Hayo wameyasema watoto wakati wa mkutano uliondaliwa na Shirika la Save the Children kupitia Ajenda ya Mtoto inayoshirikisha mashirika 30 yanayojighulisha na masuala ya watoto kwa kuwakutanisha viongozi wa vyama vya siasa na watoto ,katika kujadili nafasi ya mtoto katika ilani zao kuelekea uchaguzi mkuu uliofanyika katika Heteli ya Kebbys,jijini Dar es Salaam leo.
Mwakilishi wa Baraza la watoto la Wilaya ya Arusha Mjini,Omary Hassan amesema sheria kandamizi ya mtoto ni ya ndoa ambayo inasema mtoto wa miaka 14 anaweza kuolewa iwapo wazazi wataridhia wakati sheria hiyo inasema mtoto ni yule aliye chini ya miaka 18.
Amesema vyama vya siasa vinawajibu katika ilani zao kuweka masuala ya watoto kutokana na vyama kila vikiingia katika uchaguzi huwa havina vipengele katika ilani zao za uchaguzi vinavyolenga watoto.
Katibu Mwenezi wa Chama cha Ukombozi na Maendeleo(CHAUMA ),Eugin Kabendela amesema katika ilani za vyama kuelekea uchaguzi kuweka vipengele vya watoto vitakavyosaidia katika serikali ijayo kutoa msukumo katika masuala mbalimbali ya watoto.
Mwakilishi wa Idara ya habari na Mawasiliano wa shirika linalo shughulikia mambo ya watoto la Save the Children, Ellen Otaru akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa watoto uliowakutanisha baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa ,katika mkutano uliofanyika katika Hoteli ya Kebbys jijini Dar es Salaam leo.
Mjumbe Mwakilishi na wanahabari wa Baraza la la watoto wa Temeke Maria Miraji akitoa maada mbele ya wadau mbalimbali katika mkutano wa watoto uliofanyika katika hoteli ya Kebbys jijini Dar es Salaam leo.
Picha ya Pamoja ya watoto na baadhi ya viongozi wa vyama vya Siasa wakiwa nje hoteli ya Kebbys jijini Dar es Salaam leo. Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
Source:: Michuzi Blog
Tags
HABARI ZA KITAIFA