Unknown Unknown Author
Title: TIMU YA KATA YA MITANDI YANYAKUWA KOMBE LA RPC CUP 2014, YAIFUNGA MTANDA B 3 - 1
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
TIMU YA KATA YA MITANDI IMEIBUKA MSINDI WA MASHINDANO YA RPC CUP 2014 KWA KUIFUNGA TIMU YA MTANDA B. 3-1.   KOCHA WA TIMU YA MITANDI...
TIMU YA KATA YA MITANDI IMEIBUKA MSINDI WA MASHINDANO YA RPC CUP 2014 KWA KUIFUNGA TIMU YA MTANDA B. 3-1. 
KOCHA WA TIMU YA MITANDI AKISHANGILIA USHINDI BAADA YA KUIBUKA WASHINDI WA SHINDANO LA MPIRA WA MIGUU LA RPC CUP 2014 LILILOFANYIKA KATIKA MKOA WA LINDI NDANI YA UWANJA WA ILULU 
MASHABIKI NA WACHEZAJI WA TIMU YA MPIRA WA MIGUU YA KATA YA MITANDI WAKISHANGILIA USHINDI BAADA YA KUIFUNGA TIMU YA KATA YA MTANDA B KWA JUMLA YA MAGOLI 3 - 1 KATIKA MCHEZO WA FAINALI ULIOCHEZWA LEO JIONI KATIKA UWANJA WA ILULU.

Na.Mwandishi wetu
Timu ya Kata ya Mitandi imeinyuka Timu ya Kata ya Mtanda B kwa jumla ya magoli 3 - 1 katika kinyanganyiro cha kombe la RPC CUP 2014 mjini Lindi.
Mitandi Fc ndio ilikuwa ya kwanza kufungua kalamu ya magoli kupitia kwa mshambuliaji wake Hamisi Malinda mnamo dakika ya 7. Mtanda B waliweza kujitetea kwa kuanzisha mashabulizi langon mwa Mitandi na kuweza kusawazisha goli kupitia kwa mchezaj wake Fabian Said katika dakika ya 9, hadi kipindi cha kwanza kinamalizika timu zilitoka sare ya 1 - 1.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na timu ya Mitandi kufanikiwa kupata goli la pili kupitia kwa mshambuliaji machachali Yahaya Mkweche katika dakika ya 47. Mitandi walizidi kuliandama lango la Mtanda B nakufanikiwa kufunga bao la 3 kupitia kwa mchezaji Twaha Hassani dakika ya 81.

Hadi mwisho wa mchezo matokeo yalibaki kuwa 3-1. Hivyo timu ya Mitandi kuibuka kidedea na kunyakua kitita cha Tsh 500,000.00 na Kikombe huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Timu ya Kata ya Mtanda B na kufanikiwa kupata fedha Tsh 300,000.00 pamoja na kombe.

Nafasi ya mshindi wa tatu imeenda kwa Timu ya Kata ya MSINJAHILI na kufanikiwa kunyakuwa kiasi cha Tsh 200,000.00.

Zawadi ya Kipa bora ilikwenda kwa Saidi Mohamed wa Mitandi huku Mchezaji bora akitokea Mitandi ambaye ni Baraka Majembe. Na zawadi ya mwisho ya Mfungaji bora ikienda kwa Yusufu Hamisi wa Mtanda B wote hao waliweza kuzawadiwa fedha tasilimu kiasi cha Tsh 50,000/=

Refa wa mchezo ni Hashimu Abdallah

Mgeni Rasmi wa Mchezo huo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi Bw. Ludovic Mwananzila
Timu zikipeana Mkono Kabla ya Mchezo huo Kuchezwa
Waamuzi wa Mechi hiyo ya Fainali ya RPC CUP 2014 - LINDI

Kikosi cha Timu ya Kata ya Mtanda B kilichocheza Dhidi ya Timu ya Kata ya Mitandi katika Fainali ya RPC CUP 2014, LINDI
Kikosi cha Timu ya Kata ya Mitandi Kilichocheza dhidi ya Timu ya Kata ya Mtanda B katika Fainali ya RPC CUP 2014, LINDI
Wadau wa Michezo waliojitokeza Kudhamini Mashindano ya RPC CUP 2014 wakijadiliana mambo mbalimbali wakati wa Mchezo wa Fainali.
Mmoja wa Wadhamini wa Mashindano ya RPC CUP 2014 akipokea cheti cha Ushiriki kutoka kwa Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Lindi Ndg: Ludovic Mwananzila
Mmoja wa Wadhamini wa Mashindano ya RPC CUP 2014 Meneja wa NHIF Ndg: Fortunata Kullaya akipokea cheti cha Ushiriki kutoka kwa Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Lindi Ndg: Ludovic Mwananzila
Mmoja wa Wadhamini wa Mashindano ya RPC CUP 2014 Ndg: Alli Nalaga Kutoka Scarlet Printways akipokea cheti cha Ushiriki kutoka kwa Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Lindi Ndg: Ludovic Mwananzila
Mmoja wa Mdau wa Michezo Suleiman Mathew Diwani wa Vijibweni akipokea cheti cha Ushiriki kutoka kwa Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Lindi Ndg: Ludovic Mwananzila
Mwamuzi wa Mchezo wa Fainali ya RPC CUP 2014 Akipokea cheti kutoka kwa Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Lindi Ndg: Ludovic Mwananzila
Mwamuzi wa Mchezo wa Fainali ya RPC CUP 2014 Akipokea cheti kutoka kwa Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Lindi Ndg: Ludovic Mwananzila
Mwamuzi wa Mchezo wa Fainali ya RPC CUP 2014 Akipokea cheti kutoka kwa Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Lindi Ndg: Ludovic Mwananzila
Kipa Bora wa Michuano hiyo ya RPC CUP 2014 Saidi Mohamedi Kutoka Tiimu ya Mitandi. Akipokea zawadi yake kutoka kwa Mgeni rasmi Kitita cha Tsh 50,000/=
Mchezaji Bora wa Michuano hiyo ya RPC CUP 2014 Baraka Majembe Kutoka Timu ya Mitandi. Akipokea zawadi yake kutoka kwa Mgeni rasmi Kitita cha Tsh 50,000/=
Mfungaji Bora wa Michuano hiyo ya RPC CUP 2014 Yusuf Hamisi kutoka timu ya Mtanda B. Akipokea zawadi yake kutoka kwa Mgeni rasmi Kitita cha Tsh 50,000/=
Kaptain wa Timu ya Mtanda B akipokea zawadi ya Mshindi wa Pili kutoka kwa Mgeni rasmi Kitita cha Tsh 300,000/= na Kombe.
Timu ya Kata ya Mitandi ikipanda Jukwaani kupeana Mkono wa Pongezi na Mgeni rasmi baada ya Kuibuka washindi wa Mashindano ya RPC-CUP 2014, LINDI
Wachezaji wa Mitandi wakipeana Mkono na Mgeni rasmi
Kocha wa Mitandi akipeana Mkono na Mgeni Rasmi mara baada ya Kuibuka Washindi wa Mashindano ya RPC-CUP 2014, LINDI
Kaptain wa Timu ya Kata ya Mitandi akipokea Zawadi ya Mshindi wa Kwanza Kutoka kwa Mgeni rasmi Kitita cha Tsh 500,000/= na Kombe

Kaptain wa Timu ya Mitandi akiinua Juu Kombe la RPC - CUP kwa mashabiki wao kudhihirisha wao ndio mabingwa wa Mashindano hayo yaliomalizika hivi leo katika viwanja vya Ilulu mjini Lindi.
Timu ya Mitandi ikiwa katika picha ya Pamoja na Mashabiki wao na Kombe lao
Kocha wa Mitandi akibusu Kombe hilo mara baada ya Kukabidhiwa kama washindi baada ya kuichapa Mtanda B goli 3- 1
Shamra Shamra za mashabiki na wachezaji katika kusherehekea Ushindi wa Kombe la RPC kwa Msimu wa mwaka 2014.
Timu ya Waandishi wa Habari wakiwa wanabadilishana mawazo na Kamanda wa polisi Lindi, Kuanzia kulia ni Aisi Sobo (Startv) Ahmeid Abdulaziz (Chanel Ten & Lindi Yetu Blog) na Renatha Mzinga

About Author

Advertisement

Post a Comment Blogger

Toa Maoni Yako Kuhusu habari Hii

Note: Only a member of this blog may post a comment.

 
Top